SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, April 14, 2014

RATIBA NZIMA YA MAZISHI YA MZEE GURUMO NA SIKU ATAKAYOZIKWA


Mwanamuziki mkongwe na Gwiji la muziki wa dansi nchini Tanzania, Maalim Muhidin Gurumo,  (pichani enzi za uhai wake) aliyefariki dunia jana jioni majira ya saa 9 alasiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
 Taarifa iliyotolewa asubuhi ya leo na mtoto wa kwanza wa Marehemu Mzee Gurumo Ndg Abdallah Gurumo amesema kuwa leo saa 10 jioni kutakuwa na kisomo hapa nyumbani kwa Marehemu eneo la Tabata Kisukulu ambapo Watanzania wote wanakaribishwa. 
Baada ya kisomo saa 3 ya asubuhi kesho April 15 mwili wa Marehemu utaletwa nyumbani kwa ajili ya swala kisha saa 4 asubuhi safari ya kuelekea kijiji cha Masaki wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani itaanza kwa ajili ya maziko ya Mzee Gurumo.

Kwa mtu usiyepafamu nyumbani kwa Mzee Gurumo ukiwa unatokea Ubungo kabla ya Mwananchi kuna kituo kinaitwa Garage shukia hapo kisha ulizia mtu yoyote atakuelekeza pia kwa wewe unaetokea Tabata,Buguruni au Tazara shukia hapo Garage kituo baada ya Mwananchi.