Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba Tundu Lissu akiwasili leo kuhudhuria kikao
cha ishirini na mbili cha Bunge hilo kwenye Ukumbi mjini Dodoma.
Baadhi
ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiwasili leo kuhudhuria kikao
cha ishirini na mbili cha Bunge hilo kwenye Ukumbi mjini Dodoma.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Philemon Ndesamburo (kulia) naProfesa Kulikoyela Kahigiwakiwasili leo kuhudhuria kikao cha ishirini na mbili cha Bunge hilo kwenye Ukumbi mjini Dodoma.
Wajumbe
wa Bunge Maalum la Katiba Ismail Jussa (kushoto),Macharo Othman
Said(katikati) na Nassor Ahmed Mazrui wakiwasili leo kuhudhuria kikao
cha ishirini na mbili cha Bunge hilo kwenye Ukumbi mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta akitoa ufafanuzi
kwenye kikao cha ishirini na mbili cha Bunge hilo kwenye leo mjini
Dodoma.
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba Tundu Lissu akiwasilisha maoni ya wachache
leo kuhudhuria kikao cha ishirini na mbili cha Bunge hilo kwenye Ukumbi
mjini Dodoma.Wajumbe
wa Bunge Maalum la Katiba Anne Makinda (kushoto) na Pandu Ameir
Kificho(kulia) wakifuatilia mjadala kwenye kikao cha ishirini na mbili
cha Bunge hilo leo mjini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Kamati namba sita wa Bunge Maalum la Katiba Stephen Wassira
akiwasilisha maoni ya Kamati yake leo mjini Dodoma kwenye kikao cha
ishirini na mbili cha Bunge hilo.
Picha na Bunge Maalum la Katiba
=======
=======
KAULI ZILIZOTOLEWA BUNGENI LEO NA TUNDU LISSU, WASSIRA, MTIKILA NA ISMAIL JUSSA
Zifuatazo
ni kauli zilizotolewa na viongozi mbalimbali wa zile kamati kwenye
bunge la katiba linaloendelea sasa hivi hapa Dodoma ambapo viongozi hawa
leo April 14 2014 wameendelea kuwasilisha taarifa kutoka kwenye kamati
zao,
Ni
maoni ya pande mbili ambazo ni maoni ya wengi ambao ndio wanaounga
mkono serikali mbili alafu maoni ya wachache ambao wanaunga mkono uwepo
wa serikali tatu.
Tundu Lissu: ‘Nusu
karne ya uongo iishe, Tanganyika iliuwawa na amri za Mwalimu Nyerere na
hakuwa na mamlaka kisheria kuiua, hatujawahi kuwa nchi moja, habari ya
Tanzania kuwa nchi moja iliingizwa ktk katiba miaka 20 baada ya
muungano, nchi hii ni haramu…. miaka 50 ya kudanganyana ikome, nchi hii
inahitaji kuelezwa ukweli’
Mchungaji Mtikila:
‘tulijengwa kwenye misingi ya uongo ndio maana Mungu alishindwa
kubariki hii nchi yetu kwa miaka 50, uongo tuuondoe, swala la muungano
lilikua utapeli wa kisiasa, tuurudie ukweli kuhusu uhuru wa Watanganyika
na Wazanzibari’
Mh Wassira: ‘Hati
ya Muungano ipo, naahidi kwa niaba ya Jamuhuri itawasilishwa kwa
Mwenyekiti ndani ya siku mbili zijazo, kama Wananchi wangetoa maoni
kutaka kuvunja muungano, je tume ingeyaleta? serikali 3 italeta
mgongano’
Mh Wassira: ‘Katiba
ya Znz ndio itabakia kuwa sheria kuu kwa Znz kwa mambo yasiyokua ya
muungano, tukiweka serikali 3 hapa zikaweka masharti kuna watu watapata
matatizo, itapunguzia Wazanzibari fursa’
Ismail Jussa: ‘Hoja
za historia kwamba tulikua vipi haziwezi kulibakisha taifa katika
mgando, ukiangalia katiba ya muda ya mwaka 1965 inaendelea kuitambua
Tanganyika na kuwepo makamu wawili wa Rais’
Ismail Jussa: ‘Mkataba
wa muungano haukutoa mamlaka kwa chombo chochote kubadilisha kilichopo
ndani, ajabu bunge limefanya, tunapokua Znz tunasema mengine tukija huku
tunaufyata, Wazanzibari watatuhukumu’
Ismail Jussa:
‘Zanzibar tumeachwa watupu, tumechoka na hatukubali tena, ktk mfumo wa
serikali mbili Zanzibar haitaweza kujisimamia kamwe, hatutakubali
kuendelea nao’
Ismail Jussa: ‘Kama kuna nia njema kwa nini kuna kufichaficha, mfano mwingine hai ni Rais wa Znz kuondolewa kuwa makamu wa Rais’
CHANZO: MILLARDAYO.COM