- Ampongeza kwa ujenzi wa madaraja matatu makubwa, Daraja la Malagarasi,Kilombero na Daraja la Kigamboni.
- Ujenzi wa Sekondari za Kata
- Nape awaambia wakazi wa kijiji cha Mahembe wachague viongozi watakaotatua matatizo yao ya msingi kwanza na si vinginevyo kwani takwimu zinaonyesha viongozi wengi wa upinzani wameshindwa kutatua matatizo ya wananchi wa majimbo wanayoyaongoza.
- Wanachama wapya 160 na 7 kutoka upinzani wajiunga na CCM
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Wajumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kigoma Vijijini na kuwataka kufanya
kazi kwa umoja na mshikamano .
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya Kigoma Vijijini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wakazi wa wilaya ya
Kigoma Vijijini waliokuwa nje ya ofisi za CCM Wilaya kabala ya kuelekea
kwenye kijiji cha Mahembe ambapo mkutano mkubwa wa hadhara ulifanyika.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wananchi wa wilaya
ya Kigoma Vijijini akiwa pamoja na kiongozi wa Umoja wa Madereva na
Makondakta wa Wilaya hiyo Ndugu Mgaya Mustafa ambaye alitoa taarifa ya
kuwepo kwa kero ya kukamatwa Daladala kwa sababu ya kukosa sare za
dereva na kondakta ambazo kwa maelezo ya madereva hao tatizo lipo kwa
aliyepewa tenda kuchelewesha kushona.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji
cha Mkungwe kata ya Mahembe wilaya ya Kigoma Vijijini na kuwaambia Chama
Cha Mapinduzi kiahidi kinachoweza kutekelezeka hivyo ahadi ya kuwapatia
maji wanakijiji hao ipo na mkandarasi alishajenga mradi kwa asilimia 70
hivyo watapata maji mapema iwezekanavyo.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia mradi wa maji katika kijiji cha
Mkungwe kata ya Mahembe wilaya ya Kigoma Vijijini
Kijiji cha Mkungwe wilaya ya Kigoma Vijijini kupata maji safi na salama hivi karibuni.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha
Mahembe ambapo alitoa sifa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dk.Jakaya Mrisho Kikwete kwa kujenga madaraja makubwa matatu,Maragarasi
,Kilombero na Kivukoni na kujenga Shule za Kata nchi nzima.