SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, February 19, 2014

Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilali Afungua Rasmi Tamasha la Mwanamke na Akiba

 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Angels Moment, Bi Naima Malima akisoma hotuba ya ufunguzi wa Tamasha.
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akitoa ushuhuda wake juu ya kutumia fursa katika ujasiriamali. Mama Tunu alishiriki katika Tamasha hilo akiwa mjasiriamali aliyekuwa akiuza mazao yatokanayo na nyuki.
 Mgeni Rasmi wa Tamasha hilo, Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilali akisoma hotuba yake wakati akifungua Tamasha hilo la kwanza la kipekee kwa ajili ya wanawake na vijana.
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akimuonesha bidhaa zilizomo bandani kwake alipotembelewa na Mgeni Rasmi wa Tamasha hilo, Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilali.
 Kulikuwa na utaoji wa tuzo kwa washiriki katika Tamasha hilo. Bila kusahau burudani kutoka THT, ambao waliigiza mahudhui ya Tamasha.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Angels Moment, Bi Naima Malima akimkabidhi zawadi Mgeni Rasmi wa Tamasha hilo, Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilali.
Baadhi ya kina mama waliojitokeza kuhudhuria Tamasha hilo.

 Wake wa Viongozi (New Millenium Women Group) wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi wa Tamasha hilo, Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilali.Picha zote na Saidi Ahmed Mkabakuli

0 comments:

Post a Comment