SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, February 6, 2014

KUTOKA KWA MDAU:CLOUD 112 ATUHUMIWA KUIBA CREDIT ZA FILAMU YA DOKTA MAX.

Dr Max
 Issa Musa
Timoth Conrad - Mtayarishaji na mtunzi.
--
CLOUD 112 ATUHUMIWA KUIBA CREDIT ZA FILAMU YA DOKTA MAX. 

: AISAMBARATISHA KAMPUNI YA TIMAMU EFFECTS

Kampuni iliyokuwa inakuja kwa kasi katika tasnia ya filamu Timamu Effects ambayo inamilikiwa na Jackson Kabirigi na Timoth Conrad au maarufu kwa jina la Tico inasemekana kuwa imesambaratika kutokana na kile kilichoitwa kuwa ni hujuma kwa mmojawapo wa wamiliki hao.

Akizungumza na mtandao huu kwa masharti ya kutotajwa jina lake, msanii mmoja ambaye pia alishiriki katika kuigiza filamu hiyo alifunguka kuwa chanzo cha kusambaratika kwa kampuni hiyo ni kitendo cha Tico ambaye alikuwa mpigapicha na mhariri wa filamu hiyo kuandika kuwa filamu hiyo imeongozwa na Issa Musa au Cloud 112 ambaye ni prodyuza wa muvi hiyo badala ya Jackson Kabirigi ambaye ndiye aliongoza filamu hiyo. 

Inasemekana kuwa baada ya kuona kosa hilo  Jackson Kabirigi ambaye anang’ara na filamu ya Kisate alimkabili Tico kumuuliza kulikoni lakini badala ya Tico kufanya marekebisho alisema kuwa yeye anafuata alichoambiwa na Cloud 112 jambo ambalo ni kinyume na kanuni za filamu duniani kote kwa mtu kumpa sifa asiyestahili.
Baada ya majibizano makali kati ya wamiliki hao inasemekana kuwa kila mmoja aliamua kushika yake wakiiacha kampuni iko hewani.

Mtoa taarifa wetu aliyejibainisha kuwa anamkubali sana Kabirigi alienda mbali zaidi kwa kudai kuwa huo ulikuwa ni mpango ambao tayari ulishawekwa toka awali katika kumhujumu Kabirigi  baada ya kuonekana kung’ara katika upande wa uongozaji wa filamu hasa baada ya filamu aliyoiongoza ya Mdundiko kushinda tuzo kadhaa za kimataifa.

FC ilijitahidi kuwapata Jackson Kabirigi na Timoth Conrad bila mafanikio ila ilifanikiwa kuwasiliana na wasanii Wastara na Hidaya Njaidi ili kujua ukweli kuwa ni nani aliyeongoza filamu hiyo kati ya Jackson Kabirigi aliyeandikwa kama ‘2nd Director’ na Issa Mussa Cloud 112 aliyeandikwa kama ‘Director’  ambapo walifunguka kama ifuatavyo,

Wastara  alisema ‘’Sinema iliongozwa na Jackson Kabirigi sijui wenyewe walivyoamua, ‘’Pia aliulizwa mwigizaji mwingine ambaye ni  Hidaya Njaidi naye alifunguka hivi

 “Director ninayemjua ni Jack ambaye aliongoza filamu hiyo, kwani Cloud alikuwa na scene nyingi  za kuigiza hata kuna wakati ambao Jack alikuwa anamwelekeza akimwambia siyo hivyo fanya hivi na Cloud kutii kama jina la muongozaji kaandikwa yeye itakuwa ajabu labda walisaidiana,”anasema  Hidaya Njaidi

Bado FC inawatafuta wahusika wakuu wa habari hii, Jackson Kabirigi na Timoth Conrad. Ili kuweka sawa jambo hilo sambamba na mtayarishaji mkuu wa filamu hiyo maana siku hizi suala la Credit katika sinema linatumika vibaya.
 
 
*Habari hii imeletwa hapa na Myovela Mfwaisa
CHANZO: NA H@KI NGOWI

0 comments:

Post a Comment