Mwakilishi kutoka Ubalozi
wa Ireland nchini, Rita Bowen (wa pili kushoto) akikabidhi zawadi kwa
mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ilongelo ya
Singida, Jafari Ndagula mmoja wa washindi wawili wa jumla wa shindano
la Wanasansi Chipukizi Tanzania 2013 (YST) katika hafla iliyofanyika
jijini Dar es Salaam jana. Jafari na mwenzake Fidel Samwel (hayupo
pichani) wataiwakilisha Tanzania katika sherehe za Tuzo za kimataifa za wanasayansi chipukizi duniani mjini Dublin Ireland. Tuzo
za YST zinadhaminiwa na Ubalozi wa Ireland kwa kushirikiana na Mfuko
wa Karimjee Jivanjee Foundation (KJF). Wengine kutoka kushoto ni
Mkurugenzi wa YST, Dk. Gosbert Kamugisha na Mwenyekiti wa Mfuko wa KJF,
Hatim Karimjee.
Mwakilishi kutoka Ubalozi
wa Ireland nchini, Rita Bowen (wa pili kushoto) akikabidhi zawadi kwa
mwanafunzi wa Shule ya Fidel Castro ya Zanzibar, Muslih Othman Khamis,
mmoja wa washindi wa shindano la Wanasansi Chipukizi Tanzania 2013 (YST)
katika hafla iliyonyika jijini Dar es Salaam jana. Tuzo hizo
zinadhaminiwa na Ubalozi wa Ireland kwa kushirikiana na Mfuko wa
Karimjee Jivanjee Foundation (KJF). Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi
wa YST, Dk. Gosbert Kamugisha na Mwenyekiti wa Mfuko wa KJF, Hatim
Karimjee.
0 comments:
Post a Comment