Lionel Messi
Cristiano Ronaldo amekumbana na habari
mbaya kuelekea utoaji wa tuzo ya Ballon d'Or wiki ijayo baada ya kutoka
kwa taarifa kuhusu makubaliano ya dili baina ya adidas - wadhamini
wakuu wa Lionel Messi - na FIFA.
Katika vipengele vipya vya
makubaliano, Adidas wana haki zote za kipekee za promotion ya bidhaa za
Fifa Ballon d'Or , wakati Nike, wadhamini wakuu wa Ronaldo na mgombea
mwingine wa tuo hiyo Franck Ribery, hawana haki za kibiashara kama
ilivyo kwa Adidas kwenye tuzo hiyo.
Kwama maana hiyo inamaanisha kwamba
mshambuliaji huyo wa Real Madrid, ambaye anapewa nafasi kubwa ya kutwaa
tuzo hiyo, hatoweza kutengeneza fedha nyingi kutoka kwenye ushindi wa
tuzo hiyo kama ambavyo Messi amekuwa akitengeneza.
"Ushirikiano huu rasmi wa kibaishara
na FIFA Ballon d'or ndio sababu sisi tunaweza kutumia tuzo hii kwa ajili
ya shughuli zetu za promotion na kwa maana hiyo, kupitia makubaliano
hayo, Nike hawawezi kupata nafasi hiyo," Ben Goldhagen, Senior PR
Manager wa Adidas UK na Ireland, alisema
Adidas walitengeneza toleo maalum la
kiatu cha f50 katika kusindikiza ushindi wa nne wa Ballon d'or wa Messi
mwezi January 2013 na wamepanga kutengeneza tena kiatu hicho kwa ajili
ya Messi bila kujali matokeo ya tuzo za Ballon d'or yatakuwaje.
Ronaldo na wadhamini wake Nike,
hawaruhusiwi kisheria kutengeneza na kuuza kiatu cha namna hiyo ikiwa
nahodha huyo wa Ureno atashinda tuzo hiyo. Chanzo: shaffihdauda
0 comments:
Post a Comment