Ndugu zangu,
Naandika nikiwa Msamvu, Morogoro. Napitia vichwa vya habari magazetini na kusoma pia.
Nauona mbele mgogoro mrefu na mgumu unaoinyemelea Chadema, ni endapo viongozi wake hawatatanguliza busara na hekima.
Uamuzi wa Mahakama , mbali ya kumtendea haki Zitto una tafsiri nyingine muhi.u; kuwa mgogoro sasa unasogezwa kwenye hatua inayoweza kuufanya kuwa mrefu, mgumu na utkaozaa majeruhi na wahanga wengine wapya. Katika mazingira ya sasa linaloitwa Baraza Kuu Chadema laweza kuwa " Balaa Kuu".
Kama kweli tunaitakia mema nchi yetu na tunaamini kwa dhati katika ujenzi wa demokrasia wenye kuhitaji upinzani madhubuti, basi, tufanye jitihada za kuepusha shari kamili.
Shaaban Robert anasema; Ujana ni nusu ya uwendawazimu. Tunawaona sasa vijana wakifanya siasa kwa hulka za kiwendawazimu. Na Afrika uzee ni dawa. Ni wakati sasa wa Baraza La Wazee wa Chadema kuingilia kati haraka na kutafuta suluhu kabla hatujaona madhara zaidi ambayo kimsingi itaamanisha kushindwa kwa sisi wote, kama taifa.
Maggid Mjengwa,
Msamvu, Morogoro

0 comments:
Post a Comment