KATIBU
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa),Bwana
Jumane Sagini akiongea na waandishi wa habari muda mfupi mara baada ya
kusainiwa mkataba wa kusimamia mradi wa mabasi yaendayo haraka kati ya
Wakala wa Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam (DART) na Kampuni ya
Uholanzi ya REBEL Group jijini Dar es Salaam jana. Wengine kulia ni
Kaimu Afisa Mkuu wa DART, Bi. Asteria Mlambo na Mshauri wa Masuala ya
Fedha wa REBEL Group, Bw.Jeroen Kok (kushoto).
Kaimu
Afisa Mkuu wa DART, Bi. Asteria Mlambo(kulia) akibadilishana nyaraka za
makubaliano na Mshauri wa Masuala ya Fedha wa REBEL Group, Bw.Jeroen Kok
(kushoto) muda mfupi baada ya kusaini mkataba jijini Dar Es Salaam jana
anayeshuhudia katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa),Bwana Jumanne Sagini.
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Mradi
wa mabasi yaendayo haraka umepiga hatua nyingine baada ya kupatikana
kampuni ya washauri itakayofanya kazi ya kupatikana watoa huduma muhimu
kwa mradi huo unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwaka huu.
Hatua
hiyo imefikiwa baada ya kampuni hiyo ya REBEL Group ya Uholanzi kushinda
zabuni na kusaini mkataba wa kufanya kazi hiyo kati yake na Wakala wa
Mabasi yaendayo haraka (DART).
Katibu
Mku, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI).Bw. Jumanne Sagini aliyeshuhudia utiaji saini huo
aliwaambia waandishi wa habari mara baada ya kusainiwa kwa mkataba huo
kuwa mradi huo sasa unaelekea hatua za mwisho kabisa kuanza kufanya kazi
za usafiri wa jiji la Dar es Salaam.
Kampuni
hiyo iliyosaini mkataba na DART ilishinda zabuni miongoni mwa Kampuni
sita zilizoingia katika hatua ya mwisho ya ushindani huo.
Kwa
upande wa kampuni hiyo mkataba huo ulisainiwa na mshauri wa maswala ya
fedha,Bw. Guillaume Remy, wakati DART iliwakilishwa na Kaimu Afisa Mkuu
Mtendaji, Bi. Asteria Mlambo.
“Hatua hii ni muhimu kwa mradi huu nyeti kwa nchi yetu,” alisema Katibu Mkuu huyo.
Alisema
kutokana na kufikiwa kwa hatua hiyo, kampuni hiyo sasa itasaidia kutoa
ushauri wa jinsi ya kupatikana watoa huduma kama vile wakusanyaji nauli,
na watoa huduma wengine watakaowezesha mfumo huo kufanya kazi kwa
ufanisi.
Wadau
wengine watakaoshiriki katika mchakato huo ni pamoja na DART wenyewe,
watoa huduma za daladala na wananchi wote katika kufanikisha jambo hilo.
“Tumewaambia
wenzetu wa kampuni hii kuwa kazi hii ni nzito lakini lazima tushinde
kwa ajili ya kutoa usafiri mzuri kwa wananchi,” alisema na kuongezakuwa
swala hilo litasaidia kukabiliana na changamoto ya foleni iliyopo jijini
Dar es Salaam.
Aliitaka
kampuni hiyo kuhakikisha inafanya kazi hiyo vizuri na kuwa serikali ipo
tayari kutoa msaada pale zitakapojitokeza kero ambazo ni kikwazo kwa
utekelezaji.
Alisema
mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi
(PPP) ambapo sekta binafsi itawekeza dola za Kimarekani milioni 180 na
sekta ya umma dola za Kimarekani milioni 250.
Afisa
Mwandamizi kutoka kampuni hiyo ya Rebel Group, Bw. Jeroen Kok alisema
kampuni yao ipo tayari kufanya kazi iliyoomba ili kusaidia Tanzania
kupata huduma ya kisasa ya usafiri na kupunguza foleni ambayo ni kero
kubwa.
“Kampuni
yetu ina uzoefu wa kazi hizi ambapo tumewahi kufanya kazi Bara la
Ulaya, Asia, Ameria, Afrika ya Kusini na sasa tupo Tanzania ambayo
itakakuwa mfano mzuri katika eneo hili la Afrika juu ya utendaji wetu na
mfumo huu wa usafiri,”alisema.
Naye
Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Daladala mkoa wa Dar es Salaam
(DARCOBOA), Bw. Sabri Mabruki alisema mradi huo ni mkubwa na utasaidia
katika kufikia malengo ya serikali katika sekta ya usafirishaji jijini
Dar es Salaam.
“Sisi
wamiliki wa daladala tupo begakwabega tangu mradi huu ulipoanzishwa na
tumekuwa tukishiriki na tutaendelea kushiriki ili malengo yake yaweze
kufikiwa,”alisema Bw. Mabruki.
na michuzi matukio
0 comments:
Post a Comment