Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Barani Zanzibar Bwa.Abdi Omar
akizungumza na Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali kuhusiana na
zoezi la uokoaji lililoendelea leo asubuhi katika eneo la tukio katika
mkondo wa bahari wa Nungwi.
Sehemu
ya Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Usafiri wa Barani Zanzibar Bwa.Abdi Omar(hayupo
pichani)kuhusiana na
zoezi la uokoaji lililoendelea leo asubuhi katika eneo la tukio katika
mkondo wa bahari wa Nungwi.
---
Na Mwaandishi Wetu.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Barani Zanzibar Bwa.Abdi Omar
akizungumza na Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali kuhusiana na
zoezi la uokoaji lililoendelea jana asubuhi katika eneo la tukio katika
mkondo wa bahari wa Nungwi.
Amesema katika Na kusema katika zoezi la jana hakuna mtu yoyote
aliyepatikana wati wa zoezi hilo na zoezi hiloliloaza asubuhi ya leo
hakuna mafanikio ya kupata miili iliopata ajali hiyo, hadi mchana wa leo
hali imekuwa hivyo na bado zeizi linaendele ili kupata miili ambayo
mpaka sasa jamaa zao wamejitokeza kutokana na jamaa zao kupotea katika
maafa hayo.
Zoezi hilo linaendelea chini ya Vikosi vya Serekali na Wananchi wa Nungwi ili kupata Wananchi waliopotea katika ajali hiyo.
Amewataja Abiria waliookolewa katika ajali hiyo jana mchana ambao
wamepatikana Watu watatu ambao ni Nahir Ali Issa Mwamme mkaazi wa Mtoni
Jeshini Unguja, Ali Maulid Haji mkaazi wa mtoni jeshini Unguja na Ali
Salim Ali mkaazi wa Vitongoji kisiwani Pemba .
Pia amatowa majina ya Jamaa zaowamefika katika Idara yake kutoa taarifa
ya mpaka sasa jamaa zao hawajawaona kutoka na ajali hiyo walikuwa katika
boti hiyo ya Kilimanjaro wakitokea Pemba kwani Mohammed Khamis Said,
(13) mkaazi wa Kibweni Unguja, Najma Salum, (13) Nahid Khamis Issa, (5)
Adam Nassor Mohammed (13) Suleiman Mbarouk Salum, Mohammed Said Ali,
Sumaiya Said Ali, na Sama Ali Juma.
Mpaka sasa Wananchi wa jamaa hawa wamefika katika Ofisi za ZMA
kujitambulisha kukosa jamaa zao walikuwa katika Boti hiyo wakati
ikitokea kisiwani Pemba ikiwa katika safari zake za kawaida na kupata
mkasa wa dharuba ya upepo katika mkondo wa Nungwi na baadhi ya abiria
waliokuwa wamekaa katika sehemu ya mbele ya boti hiyo kuchukuliwa na
wimbi na kutoswa baharini.
Amesema zoezi hilolinaendelea katika jitihada za kutafuta Wananchi
waliokuwa taika Boti hiyo katika sehemu ya bahari ya Zanzibar na sehemu
nyegini ili kuhakikisha wanafanikiwa kupata Wananchi waliohusika na
ajali hiyo kukasbidhi kwa jamaa zao
0 comments:
Post a Comment