SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, January 5, 2014

Boti ya Azam II yanusurika kuzama Nungwi Leo

Pichani ni moja ya boti zinazomilikiwa na kampuni ya Bakhresa. (Picha na Maktaba).
--
Na. Andrew Chale, Zanzibar
Boti ya Azam II iliyokuwa ikitoka Pemba kwenda Unguja, leo asubuhi ilizua taharuki kwa abiria wake kufuatia kuzima ghafla kwa injini zake wakati ilipofika usawa wa Nungwi.

Kwa hali hiyo ilisababisha kizazaa kikubwa kwa abiria hao wakihofia kuzama huku wengine wakivaa majaketi maalum ya kujiokoa.

Kwa mujibu wa mashuhuda wamesema hali hiyo ilisababisha mtafaruku  mkubwa ambapo baadhi ya watu walitaka kujitupa majini.

“Chombo kilipigwa dhoruba ghafla na kusababisha kishindo kikubwa kwenda juu kwa kasi na kurudi chini kwa kishindo ndipo mlio wa injini uliposikika” Amesema Othman Omar aliyekuwa kwenye chombo hicho.

Kwa Upande wake Waziri wa Mawasiliano na Miundo Mbinu, Mh Rashid Seif ameonga na waandishi wa habari visiwani Zanzibar na kukanusha  uvumi wa kuzama kwa boti hiyo ya Azam II.

Mh. Seif amekiri kutokea kwa hitilafu katika chomgo hicho, hali iliyosababisha watu kutaharuki huku wengine wakipiga kelele za kuomba msaada.

“Unguja na maeneo mbalimbali zimezagaataarifa za kuzama, si kweli tayari chombo hicho kimefika salama Unguja na hadi sasa hakuna tukio baya” amesema Seif.
Juhudi za kutafuta Uongozi wa Bakhresa kuzungumzia tukio hili zinaendelea

Update za Ajali ya Boti ya Kilimanjaro ikitokea Pemba Leo:Abiria 3 Waokolewa na Maiti 5 zapatikana

Boti ya Kampuni ya Azam Marine ya Kilimanjaro  ikitokea Pemba asubuhi ya leo ikiwa na abiria karibu 320 imepata misukosuko ya hali ya upepo na mawimbi na kusababisha baadhi ya abiria waliokuwa wamekaa sehemu ya abiria ya mbele ya boti hiyo na kutumbukia baharini, kutoka na upepo huo.

Ajali hiyo imetokea katika mkondo wa nungwi na baadhi ya abiria wa boti hiyo kuingia baharini kutokana na mawimbi na upepouliokuwa ukivuma katika majira ya asubuhi ya leo na hali ya bahari kuchafuka.ikiwa katika safari zake za kawaidi ikitokea Pemba na kuelekea Unguja ilipata dosari kutokana na upepo na mawimbi katika maeneo ya Nungwi.

Juhudi za Wananchi na Vyombo husika kuchukua juhudi za uokoaji wa abiria hao na kufanikiwa kuwapata Wananchi watatu wakiwa hai na miili ya watu 5 kupatikana mpaka sasa.

Mpaka sasa kwa taarifa iliopatika jumla ya abiria 4 wameokolewa na kupatikana maiti 5,na zoezi la uokowaji linaendele kufanyika katika eneo la tukio  la bahari ya Nungwi. 

Maiti lzilizopatika katika zoezi hili ni 5, na mbili ni za Wanawake na tatu za Wanaume, na zoezi hilo limesitisha hadi kesho.asubuhi.Leo katika majira ya asubuhi hali ya bahari ilikuwa na mawimbi na upepo mkali 
SOURCE: H@KI NGOWI 

0 comments:

Post a Comment