Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mheshimiwa Mama Salma Kikwete akipokea tuzo ya Uongozi Uliotukuka kimataifa (Global Inspirational Leadership Award 2013) kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi Mheshimiwa Bibi Furo Giami, mwishoni mwa mkutano wa siku tatu wa Wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia. Mkutano huo ulioandaliwa na Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi (CELD), wakishirikiana na CEO Clubs Network na African Leadership Magazine uliofanyika katika hoteli ya Atlantis The Palm, huko Dubai , Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE.) Tuzo hiyo imetolewa tarehe 18.12.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba ya kushukuru mara tu baada ya kupokea Tuzo hiyo huko Dubai
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi (CELD), Bibi Furo Giami akikabidhi vyeti kwa Wake wa Marais na wanawake wengine waliotunukiwa tuzo hizo wakati wa kilele cha mkutano wa wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia uliofanyika huko Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu
Dr. Angela Moore, Balozi wa Hisani kutoka kutoka Jimbo la Georgia, nchini Marekani akiwavisha nishani washindi wa Tuzo .
Wake wa Marais kutoka Barani Afrika waliotunukiwa Tuzo na Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi wakionyesha tuzo,nishani na hati walizokabidhiwa kwa washiriki wa mkutano wa wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia na wageni wengine waliohudhuria sherehe ya utoaji tuzo hizo huko Dubai

Baadhi ya wajumbe na washiriki waliofuatana na msafara wa Mama Salma Kikwete kwenye mkutano wa wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia wakisherehekea na kumpongeza Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, wakiongozwa na Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Falme za Kiarabu Mheshimiwa Mbarouk Mbarouk, mara baada ya kukabidhiwa Tuzo ya Uongozi Uliotukuka kwenye ukumbi wa Atlantis The Palm hotel

Mama Salma Kikwete akiwa na mmoja wa wajumbe wa mkutano huo
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha na watu aliofuatana nao kwenye sherehe ya kupokea Tuzo mwishoni mwa mkutano wa siku tatu wa wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha na watu aliofuatana nao kwenye sherehe ya kupokea Tuzo mwishoni mwa mkutano wa siku tatu wa wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Mama Denise Nkurunziza, Mke wa Rais wa Burundi (kushoto) pamoja na Mke wa Rais wa Namibia Mama Penehupifo Pohamba wakati wa sherehe za kukabidhiwa tuzo za Uongozi Uliotukuka mwishoni mwa kikao cha siku tatu cha wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia kilichofanyika kwenye Hoteli ya Atlantis The Palm iliyoko Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (URA).
Picha na John Lukuwi
0 comments:
Post a Comment