SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, November 8, 2013

Daktari mstaafu hosptali ya Mawenzi akamatwa kujihusisha na utoaji Mimba

 Askari polisi wakiwa na silaha wakiwa wamezingira nyumba iliyokuwa
ikitumika kwa shughuli za kutolea Mimba.
  Daktari mstaafu wa hosptali ya rufaa ya Mawenzi Frances Shayo akiwa
mikononi mwa polisi muda mfupi baada ya kumkamata akitaka kuwatoa
mimba wasichana wawili.
 Mmiliki wa nyumba iliyoko kata ya Nga'mbo katika manispaa ya Moshi
aliyefahamika kwa jina moja la Minde akipokea kichapo toka kwa askari
polisi baada ya kukaidi kuingia kwenye gari la polisi. 
 Mmoja wa wanawake waliokutwa katika nyumba hiyo wakidaiwa kumsindikiza binti mmoja ambaye ni mwanafunzi kwenda kwa daktari huyo kutoa ujauzito.
 Msichana Irene Musa ambaye anadaiwa kuwa mwanafunzi wa shule ya
sekondari Komkwa Masama wilayani Hai akitolewa kwenye nyumba ambayo anadaiwa kwenda kutolewa ujauzito .
 Mmoja wa wanawake waliokutwa katika nyumba hiyo akidaiwa kwenda kutoa ujauzito kwa daktari huyo.
Umati wa watu waliofika katika nyumba ambayo inadaiwa kufanyika
vitendo vya kutoa mimba. Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii  Moshi.

==========   ========   ========

JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro limefanikiwa kumnasa daktari
mstaafu wa hospitali ya rufaa ya Mawenzi,mkoani Kilimanjaro, Frances
Shayo(56) akiwa katika harakati za kuwatoa mimba wanawake wawili
akiwemo Irene Musa(18) mwanafunzi wa shule ya sekondari Nkwereko
iliyoko Masama wilayani Hai.

Daktari huyo ambaye anatajwa kufanya vitendo hivyo mara kwa mara
amekamatwa  pamoja na watu wengine watano wakiwa katika nyumba ya
mkazi wa Kata ya Ng’ambo aliyefahamika kwa jina moja na  Minde.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema daktari huyo amekuwa
akifanya shughuli hiyo kwa muda mrefu katika eneo hilo na mara
nyingine amekuwa akifanya shughuli za kuwatairi watoto katika nyumba
ya rafiki yake huyo.

Akizungumza na waandishi wa habari daktari Shayo amesema msichana huyo alifika katika nyumba hiyo  akiwa na tatizo la kufunga kutokwa na damu hivyo alikuwa kwenye harakati za kutaka kumsaidia .

Kwa upande wake mama mzazi wa binti huyo,Rozi Urasa amesema alifika
nyumbani kwa daktari huyo baada ya kushauliwa na baadhi ya ndugu zake
kumpeleka kutoa ujauzito huo kutokana na kwamba huenda binti huyo

akakosa kazi pindi atakapokuwa akitafuta kazi akiwa na ujauzito.
Chanzo: na michuzi matukio blog

0 comments:

Post a Comment