SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, October 7, 2013

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli Atoa Kauli Ya Serikali Juu ya Mgomo wa Wamiliki wa Malori Tanzania Uliyoanza Leo

 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akisisitiza jambo kuhusu mgomo uliopangwa kufanywa na wadau wa usafirishaji nchini wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  leo jijini Dar Es Salaam.
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akifafanua sheria  namba 30 ya mwaka 1973 ya usalama barabarani iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2001 inayohusu kiwango cha mwisho cha uzito wa magari, kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam Kamishna Suleiman Kova akifuatilia kwa makini.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam Kamishna Suleiman Kova akieleza jinsi Jeshi la Polisi lilivyojipanga kulinda usalama ili watumiaji wa barabara wasiweze kupata usumbufu huku akisisitiza kuwa kabla ya Jeshi la polisi kuchukua hatua za kisheria ni vema vyombo vinavyosimamia usafirishaji vikachukua hatuaKushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli.
Baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Ujenzi na Waandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini maelezo toka kwa Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli.
 Picha Zote na Eliphace Marwa

0 comments:

Post a Comment