SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, October 10, 2013

Gazeti la Mwananchi Kurejea Mtaani Kwa Kishindo Kesho


Mkurugenzi wa Mwananchi, Tido Mhando akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari(Hawapo pichani) kuhusiana na kuanza kwa uchapishwaji wa gazeti hilo linalosadikiwa kuuzwa zaidi Tanzania 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications limited(MCL)Tido Mhando akizungumza na waandishi wa habari jijini kuhusu kuanza uchapishaji wa gazeti la Mwananchi kuanzia Oktoba 11, lililokuwa limefungiwa kwa wiki mbili. Kulia ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Denis Msacky na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo,Bernard Mukasa. Picha na Henry Mdimu na Dande Francis
---
Na Henry Mdimu Kampuni ya Mwananchi Communications Limited, wachapishaji na wauzaji wa magazeti ya MWANANCHI, MWANASPOTI, na THE CITIZEN leo imetoa ufafanuzi katika mambo mawili, kuhusiana na tukio lililotokea hivi karibu. Kwanza ni  gazeti lake  mama la MWANANCHI ambalo halikuchapishwa wala kuuzwa kwa takribani majuma mawili kwa agizo la serikali. Kuhusiana na hilo, wamechukua fursa na kuongelea kuhusu KUREJEA KWA UCHAPISHWAJI WA GAZETI HILO na KUUSHUKURU UMMA kwa kuwa nao bega kwa bega.

KUREJEA KWA UCHAPISHAJI WA GAZETI
Kwa mujibu wa agizo la Serikali, kutochapishwa kwa gazeti la Mwananchi kunakwisha leo, na kuanzia kesho tarehe 11.10.2013 gazeti litakuwa mitaani kama kawaida. Kwa hiyo kuanzia kesho wasomaji wa gazeti hilo maarufu wataendelea kupata gazeti lenye habari za uhakika zinazojikita kwenye umahiri, uhuru, na weledi wa uandishi na uhariri. 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw Tido Mhando, magazeti hayo yataendelea kusambazwa nchi nzima na kufika mapema kabisa kote, kupitia kwa mawakala na wauzaji wake walioenea kote Tanzania.

Kwa wapenzi wa gazeti la Mwananchi waliopo jijini Dar es Salaam, kesho watauziwa magazeti na waandishi wa gazeti hilo ambao kuanzia asubuhi watakuwa mtaani wakisherehekea uhuru wao kwa kukutana na wasomaji wao moja kwa moja.

PROMOSHENI YA CHOMOKA NA MWANANCHI
Kutochapishwa kwa gazeti la MWANANCHI kwa majuma mawili kulisababisha ile promosheni yaCHOMOKA NA MWANANCHI isimame kwa muda huo huo. Tido alichukua Fursa kuwajulisha wasomaji wake kwamba promosheni hii sasa inarudi tena na inaendelea kuanzia ilipokuwa imekomea. Zawadi za shilingi milioni moja kila siku, na zawadi za magari mapya, zitaendelea kushindaniwa na kutolewa ili kutimiza ile ahadi yetu ya kutoa zawadi zenye thamani ya jumla ya shilingi 250,000,000/=.

0 comments:

Post a Comment