
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akimpa zawadi ya kinyago cha umoja meya wa mji wa Vallejo Mtahiki Osby
Davis wakati wa sherehe ya kumbukumbu ya miaka ishirini ya ushirikiano
kati ya mji huo na mji wa Bagamoyo


Meya wa Mji wa Vallejo lililopo
katika jimbo la California nchini Marekani Mstahiki Osby Davis
akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa mji huo
leo tayari kwa sherehe za kumbukumbu ya mwaka wa ishirini ya ushirikiano
kati ya mji huo na mji wa Bagamoyo.

Mjumbe wa Kamati ya ushirikiano
kati ya mji wa Vallejo na mji wa Bagamoyo Bi Dinah Villanueva akikabidhi
kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete hati ya kumbukumbu ya kuanzishwa kwa
ushirikiano kati ya mji wa Vallejo na Bagamoyo miaka ishirini
iliyopita.Ushirikiano huo uliasisiwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akiwa Waziri wa Nishati na Madini na mbunge pamoja na kamati ya wajumbe
kutoka mji wa Vallejo California. Katikati akishuhudia ni Meya wa mji wa
Vallejo Mstahiki Osby Davis.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akisalimiana na baadhi ya Watanzania waishio katika mji wa Vallejo jimbo
la California nchini Marekani leo wakati Rais alipotembelea mji huo wa
kibiashara kwa mwaliko wa meya wa mji huo Mstahiki Osby Davis.
Picha na Freddy Maro IKULU
Picha na Freddy Maro IKULU




0 comments:
Post a Comment