
Paroko wa Parokia ya Roho Mtakatifu Cheju Zanzibar, akisaidiwa na
Frateri, Richard Haki kupumzika kitandani baada ya kuzungumza na
waandishi katika katika Wodi ya Kibasila iliyopo katika Hosipitali ya
Taifa ya Muhimbili (MNH) jijni Dar es Salaam jana.Picha Salim Shao
****
Padri wa Parokia ya Mpendae ya Kanisa Katoliki Zanzibar, Anselmo
Mwang’amba amesema kuwa alimwona mtu aliyemwagia tindikali na
kumsababishia majeraha na kueleza kuwa anashangaa kuona polisi
hawajamkamata hadi sasa.
Akizungumza jana katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, kwenye Wodi namba 16, Kibasila alipolazwa, Padri Mwang’amba
alisema baada ya kumwagiwa tindikali, alimwona mtu huyo akikimbia
kuelekea katika nyumba moja jirani.
“Kwa kuwa mimi nilikuwa na taharuki na maumivu,
sikuweza kuendelea kumfuatilia, ila dereva aliyenikimbilia kunipa msaada
aliniambia kwamba alimwona mhusika akikatiza kwenye uchochoro hadi
alipoingia kujificha kwenye nyumba iliyopo jirani na eneo hilo,” alisema.
Kwa habari zaidi Bofya na Endelea.===.>>




0 comments:
Post a Comment