SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, May 19, 2013

YANGA YAIGONGA SIMBA 2-0, Yatwaa kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara Jana

Nahodha wa Yanga, Nidir Haroub 'Canavaro' akiwa amenyanyua kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara pamoja na wachezaji wenzakeya Simba SC.

****
 Timu ya Yanga jana imewaadhibu watani wao wa jadi, Simba SC baada ya kuwalaza kwa bao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mabao ya Yanga yamefungwa na Didier Kavumbagu na Hamis Kiiza. Baada ya mchezo huo, Yanga SC ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara Jana

Beki wa Simba, Musa Mudde (kushoto) akichuana na mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo. 


Beki wa Simba, Shamte Ramadhani akimtoka mshambuliji wa Yanga, Simon Msuva
Shabiki wa Yanga akipelekwa kupewa huduma ya kwanza baada ya kuzimia wakati mchezo ukiendelea.
Kikosi cha Simba.
Makocha wa yanga wakipanga mikakati ya Ushindi.
Timu zikiingia uwanjani.
Timu zikisalimiana.
Kocha wa Simba, Kibabu Patrick Liewig
Kocha wa Yanga, Ernst Brandts
Beki wa Simba, Shomari Kapombe akimtoka mshambuliji wa Yanga, Simon Msuva
Msanii Juma Nature akitumbuiza wakati wa mchezo huo.
Kumbe naye Yanga!
Mshambuliaji wa Simba, Felix Sunzu akitafuta mbinu za kuwatoka mabeki wa Yanga. Lakini wapi.....
Mashabiki wa Yanga.
 Raha ya ushindi.
 Kocha wa Yanga, Ernst Brandts akiwa amebebwa na wachezaji wake.
 Kiduku kikiongozwa na kocha msaidizi Fred Felix Kataraia Minziro (shoto)
KARIBU JANGWANI NGASA
Mashabiki wa Yanga wakiwa wamembeba mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngasa mara baada ya mpira kumalizika, ikiwa ni ishara ya kumkaribisha katika klabu yao. 
Mashabiki wa Yanga kwa vituko... aha! Hapa Simba kaolewa...
Wachezaji wa timu ya Yanga wakishangilia ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kuifunga Simba 2-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa  jijini Dar es Salaam
Kipa wa Simba, Juma Kaseja akijaribu bila mafanikio kuokoa mpira wa kichwa uliopigwa na mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu, kuandika bao la kwanza  katika mchezo wa kufunga pazia la Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
KARIBU NYUMBANI
Mashabiki wa Yanga wakiwa wamembeba mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngasa mara baada ya mpira kumalizika, ikiwa ni ishara ya kumkaribisha katika klabu yao. 
Refa wa mechi ya Simba na Yanga, Nartin Saanya akiwa chini baada ya kugongwa kwa bahati mbaya na mchezaji wa Yanga, Didier Kavumbagu.
Refa, Martin Saanya akipata matibabu baada yakugongwa kwa bahati mbaya na  mchezaji wa Yanga, Didier Kavumbagu. Picha na Francis Dande
 Wachezaji wa Yanga wakishangilia huku wakiwa na Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara walilokabidhiwa baada ya kuwabwaga watani wao wa jadi Simba mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

 Binti shabiki wa Yanga akishangilia huku akiwa na kombe bandia
 Yanga wakishangilia bao la kwanza dhidi ya Simba lililofungwa na Kavumbagu katika dakika ya tano kipindi cha kwanza
 Yanga wakishangilia bao
 Mwamuzi Martine Saanya wa mechi ya watani wa jadi Yanga na Simba, akiwa chini baada ya kugongana kwa bahati mbaya na mchezaji Kavumbagu wa Yanga wakati wa alipokwenda kuamulia ugomvi.
 Kocha msaidizi wa Simba Jamhuri Kihwelu 'Julio' akiteta jambo na Nahodha wa Yanga Haroub Canavaro baada ye mechi kumalizika
 Benchi la Simba likiwa hoi baada ya kufungwa bao lapili na Yanga
 Kocha wa Yanga akiwa amebebwa na wachezaji walipokuwa wakishangilia ubingwa
 Yanga wakishangilia kianika
 Yanga wakivishwa medali za ushindi 
 Kavumbagu wa Yanga akifunga kwa kichwa bao la kwanza dhidi ya Simba
                                                                    Simba lazima achinjwe
 Simba wakiwa na furaha kabla ya kufungwa na watani wao wa jadi Yanga
 Mashabiki wa Yanga (kulia) na wa Simba kushoto
 Yanga ni nderemo kila mahala
Kipa wa Yanga, Ali Mustapher 'Barthez' akirushwa juu ya wachezaji wenzie wakati wakishangilia ushindi  wa mabao 2-0 dhidi ya watani wao wa jadi Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA

0 comments:

Post a Comment