Gari aina ya Noah likiwa limegandamizwa na zege.
Hii ndiyo hali halisi ya tukio lilivyokuwa.
Gari aina ya Toyota likiwa limebonyezwa na zege.
Hali ilikuwa ni mbaya katika zahama hiyo ya alfajiri ya leo.
Watu wakiangalia magari yao.
SEHEMU ya ukuta wa kituo cha mabasi ya kwenda mikoani cha Ubungo, jijini Dar es Salaam, leo alfajiri umeanguka na kuyaharibu vibaya magari zaidi ya ishirini yaliyokuwa yameegeshwa nje ya eneo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela alisema kuwa idadi ya magari yaliyopatwa na ajali hiyo yanakadiriwa kufikia 24 ambapo watu watatu wanasemekana wamejeruhiwa.
Habari/Picha: Musa Mateja/GPL




0 comments:
Post a Comment