SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, October 13, 2012

TAFRIJA YA NBC KWA WAJUMBE WA MKUTANO WA 22 WA PPF YAFANA

 Afisa wa Mfuko wa Pensheni nwa PPF, Mkoani Arusha, (Kulia), akipoz kwa picha na mwandishi habari wa Channel Ten mkoani humo, Jamila Omar, wakati wa cocktail party iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa ajili ya wajumbe wanaohudhuria mkutano wa 22 wa wanachama na wadau wa Mfuko wa Pensheni wan PPF Alhamisi usiku Oktoba 11, 2012, kwenye hoteli ya Kibo Palace jijini humo. Mkutano bhuo wa siku tatu uliowaleta pamoja zaidi ya wajumbe 700 kutoka ndani na nje ya nchi, utakamilika Ijumaa Oktoba 12, 2012
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (Kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa NBC, Lawrence Mafuru, (Katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemiah Mchechu, wakibadilishana mawazo kwenye tafrija hiyo iliyoandaliwa na NBC kwa wajumbe wanaoshiriki mkutano wa 22 wa wanachama na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, mjini Arusha.
 Mhariri Mtendaji wa gazeti la Nipashe Jumapili, Flora Wingia, (Kulia), Jane Mihanji, (Wapili kulia), wakiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, David Mattaka
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dkt. Ramadhan Dau, (Wapili kulia), akiwa na viongozi wa Jukwaa la Wahariri, Mwenyekiti, Absalom Kibanda, (Kulia), Katibu wake, Nivile Meena na mgeni mwingine mwalikwa
 Wafanyakazi wa PPF na wageni wengine waalikwa wakiwa katika poz
 Mshereheshaji mashuhuri nchini, Mzee Mavunde, (Kushoto), akijiunga kwenye picha na wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, katika picha hii ya kumbukumbu
Baada ya ushiriki wa siku mbili mfululizo kwenye mkutano huo, Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF ambaye pia ndio mratibu wa mkutano wa 22 wa wanachama na wadau wa mfuko huo, Lulu Mengele, (Katikati), akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wenzake, kwenye tafrija hiyo iliyoandaliwa na NBC.

0 comments:

Post a Comment