


Picha juu na chini ni washaktakiwa zaidi ya 50 wakiwa pamoja na Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam,Sheikh Issa Ponda wakiwa ndani ya karandimnga la polisi

Baadhi ya akina mama wanaounganishwa kwenye mashtaka hayo pamoja na Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam,Sheikh Issa Ponda

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam,Sheikh Issa Ponda (wa tatu kulia)leo akiwa ndani ya mahakam ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo na wenzake 50 kujibu mashtaka mbalimbali pamoja na kuwashawishi baadhi ya Waislamu kuvamia eneo la Kiwanja katika eneo la Chang'ombe jijini Dar es Salaam, kuwashawishi Waislamu kutojitokeza katika zoezi la Uandikishaji katika Sensa ya Watu na Makazi.
VIDEO:
Kiongozi wa jumuiya na taasisi za kiislam Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda na wafuasi wake wapatao 49 waliokamatwa na jeshi la polisi jijini Dar es Salaam kutokana na tuhuma mbalimbali wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu ambapo wote kwa pamoja wamesomewa mashtaka manne huku shekhe Ponda akisomewa mashtaka matano likiwemo la uchochezi wenye kuhamasisha utendaji wa makosa yanayoweza kuhatarisha usalama.




0 comments:
Post a Comment