Rais wa Wanafunzi Waislam, Jafari Mneto akizungumza katika viwanja vya Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam baada ya Wanafunzi Waislam kufanya maandamano ya amani.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa akizungumza na wanafunzi.
-------
Tangazo la taarifa ya kusudio la kuandamana ilitangazwa kwenye vyombo vya habari ikiwemo hapa BOFYA. Maandamano yamefanyika katika maeneo kadhaa nchini. Ifuatayo ni taarifa toka Morogoro na picha za Dar es Salaam na Morogoro.
*******
Mamia ya Waislamu wa Morogoro wakiwemo Wanafunzi na Vijana wa Kiislamu wameandamana hadi Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuwasilisha madai yao mbalimbali yakiwemo ya kupinga mfumo Kristo ndani ya Serikali.
Maandamano hayo yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi na Vijana wa Kiislamu Mkoa wa Morogoro, yalianza mara baada ya swala Ijumaa kutoka Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro eneo la Msamvu , kupitia katikati ya mitaa ya Manispaa ya Morogoro hadi nje ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa .
Hivyo pamoja na kufikisha risala hiyo, wameipa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa siku 21 kuanzia Januari 20, mwaka huu kuyashughulikia madai ya Waislamu wa Mkoa wa Morogoro na kupatia uvumbuzi wa kudumu, vinginevyo watayashughulikia wao wenyewe.
Wakati maaandamano hayo kijumuisha baadhi ya wasilamu wengine njiani , Polisi Mkoa wa Morogoro chini ya Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Joseph Rugira, waliwahi kuziba njia karibu na Ikulu ndogo yakiwemo na Makazi ya Mkuu wa Mkoa sambamba na lango la kuingilia Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
Hata hivyo wakati maandamano hayo wakisika kasi kwa waislamu hao kubeba mabango yaliyoanzidikwa ‘Kupinga mazira mfumo kristo Tanzania’ ‘No Peace without justice ‘pia walibeba mabango yaliyoandikwa kwa vitambaa yakiwa na ujumbe ‘Majengo ya Serikali Ardhi ya Kanisa . JK Thibitisha …lazima kieleweke’ na ‘ Pasipo haki hakuna usawa’.
Azma ya kufanyika kwa maandamano hayo ni kushinikiza Serikali kuuondoa mfumo kristo , kudhulumiwa , kunyanyaswa na ukandamizaji wa wanafunzi wa Kiislamu mashuleni, Vyuoni na kubakizwa nyuma kwa makusudi katika elimu , ajira na maeneo mengine mbalimbali na kupewa majina mabaya kama magaidi ili kuhalalisha dhuluma dhidi ya Waaislamu.
Pamoja na kurupushani hizo, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Rugira, aliwataka Waandamanaji hao kuteua wawakilishi watano wataowasilisha risala yao kwa Mkuu wa Mkoa na wao wabakie wakisubiri kupatwa majawabu.
Hatua hiyo iiliafikiwa na Waaislamu hao, na waliwateua wawakilishi watano kupeleka ujumbe katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa , ambapo pamoja na kufika Ofisi hiyo, Mkuu wa Mkoa alikuwa safarini na wao wakimtaka Ofisa Elimu wa Mkoa ili asikilize madai yao.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Mgeni Baruani, aliazimika kutoka nje ya lango kuu walipokuwa wameketi waandamanaji hao ili kusikiliza risala yao iliyosomwa na Shehe Mohammed Mohammed , ambaye pia alikuwa ni Mratibu na Msemaji wa Maandanano hayo.
Katika risala yao, walidai kuwa Serikali ya Tanzania haiwathamini Waislamu wala kujali shida zao , pamoja na sauti za vilio na hivyo kutoa tamko la kuitaka Serikali kuu na Mkoa iwachukulie hatua za kisheria wanafunzi, walimu, watendaji wanaongoza kuleta migogoro ya Kidini Shuleni na sehemu za kazi.
Hata hivyo katika mambo yao sita ni kuwa watapambana wenyewe watakapoona wanadhulumiwa katika kutetea haki kwa vile ni wajibu wa waislamu kufanya hivyo na kwamba huo ndiyo msimamo wao wa kuueneza nchini kote hadi pake Serikali itakapoonesha kujali na kudhamini waislamu.
Akizungumza baada ya kupokea risala ya madai yao, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Baruani, aliwataka Waislamu hao kuwa watulivu na kwamba Mkuu wa Mkoa mara atakaporejea atakabidhiwa ili kuyapitia na yenye kuhitaji kuchukua hatua zaidi ya kuwasilisha kwa Rais Jakaya Kikwete.
Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Rugira, ambaye pamoja na safu yake walijitahidi kuzungunza na baadhi ya viongozi wa Maandamani hayo kuwataka watulize jazba na baada ya kuwasilisha kilio chao aliwataka watawanyike kwa amani na utulivu.
Hata hivyo kabla ya kutawanyika walimtaka Kaimu Kamanda huyo wa Polisi, kuwaachia wenzao watatu waliokamatwa kwa madai ya vinara wa maandamano hayo na dai lao lilikubaliwa na kuwawachia Siamini Said, Athuman Seba na mwanamke mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja.
Lakini Waislamu hao walitaka Jeshi la Polisi limlipe fidia mmoja wao aliyetambuliwa kwa jina la Mgeni Athumani aliyepasukiwa na bomu sehemu ya kichwani na kusababisha majeraha. Hata hiviyo Waislamu hao mara baada ya kuwasilisha madai yao walitii agizo la kuwataka kutawanyika eneo la Ofisi za Mkuu wa Mkoa na waliodoka kwa amani majira ya saa kumi jioni kurejea kuendelea na shughuli zao nyingine.
0 comments:
Post a Comment