Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Bwana Joseph Mbilinyi akiwasihi wananchi kuwa watulivu na kwamba mgogoro umekwisha na utatuliwe kisayansi badala ya kisiasa na pia amewapongeza machinga kwa utulivu waliouonyesha bila kupora bidhaa madukani.
Halaiki ya wananchi waliofika kuusikiliza mustakabali wa wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama machinga kuendelea na biashara zao katika maeneo yao ya awali, wakati utaratibu wa maeneo ya kufanyia biashara ukiandaliwa na halmashauri ya jiji la Mbeya.
Maelfu ya wananchi waliofika kuusikiliza mustakabali wa wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama machinga kuendelea na biashara zao katika maeneo yao ya awali, wakati utaratibu ukiandaliwa na halmashauri ya jiji la Mbeya.
Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), likiwasaidia Jeshi la Polisi kuweka hali ya amani na utulivu mara baada ya kuisha kwa mkutano uliofanyika katika kituo cha mabasi madogo ya abiria (daladala) eneo la Kabwe Mwanjelwa jijini Mbeya.
Credit To H@ki Ngowi




0 comments:
Post a Comment