SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, October 27, 2011

MAAJABU MAZISHI YA MUAMMAR GADDAFI

 Muammar Gaddafi
Luqman Maloto na Intaneti
MAZISHI ya aliyekuwa Kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi, yalitawaliwa na maajabu ya aina yake, kubwa zaidi likiwa ni kaburi alilozikwa kuwa na kina kirefu kupita kawaida.
Hata hivyo, haikuelezwa ni muda gani mwili wa Gaddafi ulizikwa lakini vyanzo mbalimbali vinaeleza maajabu ya mazishi hayo.

MOSI: Kaburi hilo lilichimbwa urefu wa futi 12.  Baraza la Mpito la Libya (NTC) lilifanya makusudi ili kuwakomoa watu watakaotaka kuutafuta mwili wa kiongozi huyo.

PILI: Alizikwa wakati wa giza. Walifanya hivyo ili watu wasione. Lengo ni sehemu aliyozikwa ibaki kuwa siri.

TATU: Inadaiwa hakuoshwa kama sheria ya dini yake ya Kiislam inavyotaka, wala hakuhifadhiwa kwenye sanda.

NNE: Hakuna ndugu yeyote aliyehudhuria.

TANO: Hakukuwa na kiongozi wa kidini aliyeongoza mazishi. Wapiganaji wa NTC kwa muongozo wa mabosi wao, waliuchukua mwili wake na kuufukia.

AZIKWA JANGWANI
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kama lilivyopokea taarifa kutoka kwa maofisa wa NTC, jirani na Gaddafi alizikwa mwanaye aliyeuawa naye wakati wa mapambano, Mutassim.

BBC liliandika kuwa NTC ilieleza kwamba Gaddafi alizikwa jangwani kwa siri mno na hakuna alama yoyote ambayo imeachwa.

Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa serikali ya Gaddafi, Libya, Abu Bakr Younis Jabr, ambaye aliuawa siku moja na bosi wake, alizikwa pia sehemu hiyo.

MWISHO MBAYA
Ulikuwa mwisho mbaya wa Kanali Gaddafi, kwani kabla hajazikwa, mwili wake ulikuwa umeshaharibika na kutoa wadudu.

Habari zinasema kuwa wananchi wa Libya, waliokuwa wanakwenda kuushuhudia mwili huo walilazimika kufunika pua zao kutokana na harufu kali.
Habari Zaidi Endelea======>>

0 comments:

Post a Comment