SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, June 20, 2011

WAZIRI MKUU AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UTUMISHI WA UMMA JIJINI DAR!!

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akifungua kongamano la siku nne wa kimataifa wa utumishi wa umma leo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Mawaziri wa Utumishi wa Afrika ambaye pia ni Waziri wa Utumishi wa Kenya Dalmas Otieno Anyango akitoa ufafanuzi juu ya viongozi wa Afrika kuacha tabia ya kurithishana uongozi kutoka mzazi hadi mtoto. Waziri huyo alitoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam katika kongamano la kimataifa la utumishi wa umma.
Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda (kulia) akibadilishana mawazo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Hawa Ghasia wakati wa kongamano la kimataifa la utumishi wa umma liloanza leo jijini Dar es salaam. Waziri Mkuu alikuwa ngeni rasmi katika ufunguaji wa kongamano hilo.
Washiriki  wa Kongamano la Kimataifa la utumishi wa umma wakimsilikiliza Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda (hayupo) pichani wakati wa ufunguaji wa kongamano hilo jijini Dar es  Salaam.
(Picha na Tiganya Vicent-MAELEZO Dar).

0 comments:

Post a Comment