SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, June 7, 2011

RAIS WA UGANDA KULIHUTUBIA TAIFA LEO!!

Rais Yoweri Museveni.
Rais Yoweri Museveni wa Uganda leo analihutubia taifa katika ukumbu wa bunge kuzungumzia masuala muhimu na msimamo wan chi hiyo.
Hotuba kama hiyo hutolewa mara moja katika mwaka kila mwanzoni mwa mikutano ya bunge, na hutolewa kuzungumzia suala lolote lenye umuhimu kwa taifa.
Rais huyo atazungumzia masuala mbali mbali ikiwemo kutoa ufafanuzi juu ya suala la kukua kwa uchumi, kuongezeka kwa gharama za maisha na mfumuko wa bei.
Waziri wa Habari Mary Karooro Okurut amesema rais Museveni ataelezea suala la nishari na mtandao wa barabara ikiwa ni pamoja na elimu na sekta ya afya.
Amesema rais pia atazungumzia mapungufu yaliyopo katika utoaji huduma katika sekta za elimu na afya, na kuongezea kuwa sehemu kubwa ya ahadi zilizotolewa mwaka jana zimetimizwa.
Mwaka jana rais Museveni aliahidi kukua kwa kasi kwa uchumi, kuimarishwa kwa vita dhidi ya rushwa na kujenga bwawa la kuzalisha umeme la Bujagali litakalozalisha MegaWati 250.
WAKATI HUO HUO
Rais Yoweri Museveni amewatahadharisha mawaziri wapya nchini humo dhidi ya tabia ya majivuno.
Amesema tabia hiyo ni moja ya mambo yanayosababisha kuvunja umoja miongoni mwa makada wa chama tawala cha National Resistance Movement (NRM).
Aidha amefafanua kuwa aliangalia kigezo cha uwezo wa upatanishi na kujenga umoja wakati akiunda baraza jipya la mawaziri.

0 comments:

Post a Comment