SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, May 21, 2011

MWISHO WA DUNIA..........KULIKONI!!!!!?????

Naomba Tafakari Juu Ya Uvumi Wa Suala Hili Mdau!!!
Habari zenu wadau wote wa 24 SEVEN 365 popote pale mlipo duniani mkifuatilia blog hii ya Jamii.
Nimeguswa sana na suala hili la huyu mchungaji kutabiri mwisho wa dunia Mei 21 2011.
Alishawahi kutabiri mwisho wa dunia mwaka 94. Ni kudanganya waumini tu, Kesho akiongea jambo je waumini watamuamini tena!!??
Kwanza kabisa nijuavyo mimi ni kuwa hapa duniani hakuna mwanaadam hata mmoja ajuaye siri ya M/Mungu, kujua lini,muda gani na mwaka gani utakuwa mwisho wa dunia ni mungu pekee ndie ajuae na si mwanaadam.
Pili katika vitabu vitukufu vya mungu kuna dalili ambazo zimeelezwa pindi utapokaribia mwisho wa dunia zimeanza kuonekana na nyingine bado hazijadhihiri.
Miongoni mwa hizo ni Manabii Wa Uongo,ilitabiriwa ya kwamba utapokaribia mwisho wa dunia watakuja manabii wengi wa uongo na kutumia mwamvuli wa dini kwa kujifanya wametumwa na Mungu kuja kuitangaza dini hali yakuwa si wa kweli yaani manabii feki.
Kwa muono wangu naona huyo mchungaji na utabiri wake huo ni moja kati ya zile dalili zilizotabiriwa na kuelezwa katika vitabu vya Mungu.
Wakati umefika sasa ya Mungu mwachie Mungu..................................!!!!!
Yatosha!!
Nawatakia kila la heri na Mungu awabariki.
Asante.
Mdau wa 24 SEVEN 365 "Harakati Hazikomi".

0 comments:

Post a Comment