SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, April 30, 2011

VODACOM TANZANIA YAZINDUA RASMI SHINDANO LA UREMBO LA VODACOM MISS TANZANIA KWA MWAKA 2011

Mkuu wa Udhamini wa Kampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania, Bw. George Rwehumbiza akizungumza katika hafla fupi ya kuzindua rasmi shindano la Urembo la Vodacom Tanzania kwa mwaka 2011 wakiendelea kuwa wadhamini wakuu wa shindano hilo. Bw. Rwehumbiza alisema kwamba shindano la mwaka huu lina mvuto wa aina yake kwani warembo thelathini watakaoingia fainali hawataweka kambi hotelini kama ilivyozoeleka na watakaa kwenye nyumba maalum itakayojulikana kama nyumba ya Vodacom.
Walioketi kutoka kushoto ni Mratibu wa Majaji wa kamati ya Miss Tanzania Dr. Ramesh Shah, Mkurugenzi Mtendaji wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga, Mkuu wa Udhamini Vodacom Tanzania George Rwehumbiza, pamoja na Mkuu wa Itifaki ya Kamati ya Miss Tanzania Albert Makoye katika picha ya kumbukumbu na warembo mara baada ya uzinduzi.
Miss Tanzania 2007 Richa Adhia akiwa na mume wake mtarajiwa Hridhaan Dhillon.
Meneja Udhamini na Promotion wa Vodacom Bi. Rukia Mtingwa akimsikiliza kwa umakini Brother Ben Kisaka wa Jambo leo wakati wa kubadilishana mawazo katika hafla hiyo. Wengine ni Mkurugenzi wa T.H.T Ruge Mutahaba na Mkurugenzi Mtendaji wa Gazeti la Jambo leo na Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto.
Aba Billdard kutoka Vodacom akiwa na mdau katika pozi.
Mbunifu wa Mavazi Ally Rehmtullah akiwa na Warembo waliowahi kutwaa taji la Miss Tanzania.
Wadau wakila wakinywa na kubadilishana mawazo katika hafla hiyo Linkiliyofanyika katika Hotel ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es Salaam.
Na Mo Blog.

0 comments:

Post a Comment