SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, April 29, 2011

SERIKALI KUANZA KUWATUMIA WAKANDARASI WAZALENDO KATIKA UJENZI WA BARABARA

Naibu Waziri wa Ujenzi Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza kwenye kikao na watendaji wa mkoa wa Singida.
Na.Nathaniel Limu, Singida.
Naibu Waziri wa Ujenzi Dk. Harrison Mwakyembe (Mb) amesema serikali inaandaa mkakati wa kupunguza gharama kubwa za ujenzi wa barabara zinazotozwa hivi sasa na makandarasi kutoka nje ya nchi.
Amesema kuendelea kulipa gharama hizo kubwa pamoja na kutekeleza masharti yanayotolewa na makandarasi hao hakutafanikisha lengo la serikali la kuwa na barabara nyingi za lami nchini.
Dk. Mwakyembe amesema hayo muda mfupi baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa ujenzi na uboreshaji wa barabara mkoani Singida iliyotolewa na meneja wa TANROADS mkoa Mhandisi Yustaki Kangole.
Akifafanua amesema makandarasi hao kutoka nje ya nchi wamepandisha mno gharama ya ujenzi wa barabara za lami, kutoka shilingi milioni 350 kwa kilomita moja mwaka 2005/2006 hadi shilingi bilioni 1.5.
Aidha Naibu Waziri huyo amesema sasa msisitizo mkubwa utaelekezwa katika kuwapatia kazi ya ujenzi makandarasi wazalendo ambao pamoja na mambo mengine wana uchunLinkgu na nchi yao.
Katika hatua nyingine Dk. Mwakyembe amesema pamoja na kushughulikia suala la kushusha gharama za ujenzi wa barabara, pia watachunguza na kufanya mabadiliko makubwa katika mikataba ambayo mingi, amedai haiionei uchungu nchi hii.
Wakati huo huo amewataka wafanyakazi waliochini ya wizara ya ujenzi kurejesha uadilifu na weledi ili kazi zinazofanywa na kusimamiwa ziwe bora kwa mujibu wa mikataba husika na ziweze kudumu kwa muda mrefu.
Na Mo Blog.

0 comments:

Post a Comment