SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, April 29, 2011

Rais wa Shirika La Under The Same Sun Akiongea Na Watu Wenye Ulemavu Wa Ngozi Jana

Rais wa Shirika la Kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi linalofahamika kwa jina la UNDER THE SAME SUN,Peter Ash akizungumza jioni ya jana na baadhi ya watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na wanahabari huku Mkurugenzi wa Shirika hilo hapa nchini,Vicky Ntetema akimsaidia kutafsiri kwa kiswahili ili kuwaelewesha wale wasiojua lugha la kiingereza.hii ni katika hafla ya mkutano na watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Nyumbani Hotel,jijini Mwanza.Mkuu wa Wilaya ya Misungungwi,Mh. Mariam Lugairwa akizungumza katika mkutano huo jioni ya jana,ambapo aliwataka watu kujituma katika kufanya kazi ili kufanikiwa katika maisha na si kuweka dhana potofu ya kusema kwamba ili mtu afanikiwe kimaisha basi li lazima apate viungo vya albino.hii ni jioni ya leo katika hafla iliyoandaliwa na shirika la UNDER THE SAME SUN katika hoteli ya Nyumbani,jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ulemavu wa Ngozi Mkoani Mwanza,Alfred Kapole akizungumza wakati akifungua mkutano huo jioni ya leo.
Maafisa wa Shirika la UNDER THE SAME SUN kutoka jijini Dar wakibandika baadi ya picha ukumbini hapo.
Watoto wenye ulemavu wa ngozi ambao walihudhulia hafla mkutano kati ya Shirika la UNDER THE SAME SUN na watu wenye ulemavu wa ngozi.
Mwanalibeneke wa Libeneke la G. SENGO,Albert Sengo akiwa bize kuandika yaliyokuwa yakijiri ndani ya mkutano huo.
Na matukio michuzi

0 comments:

Post a Comment