SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, April 13, 2011

Q-JAY AIMWAGA BONGO FLAVA!

Mkali wa RnB Tanzania ambaye kwa sasa anaendelea kula matunda ya ndoa,Joseph Kelvin Mapunda aka Q-Jay kwa sasa ameokoka na kuamua kumfuata Bwana
Q-Jay amekuwa akitolea nje concert kibao ambazo anaalikwa kwa ajili ya kufanya show,kutokana na imani yake mpya aliyonayo sasa,na amefunguka kuwa “mziki niliokua nafanya ulikua ni wa dunia na ningewashauri wasanii wenzangu wote wanaoimba nyimbo za dunia kuufata wokovu na kuachana nazo,kwa sasa nimepumzika kufanya shughuli za mziki lakini kuanzia mwezi wa sita nitaanza kurekodi mziki yangu mipya ya kumtukuza mungu yaani gospel na natarajia kutoa album”....alimalizia Q Jay kwa sauti pole ya kilokole,akifuata nyayo za Stara Thomas,K Basil na Renee Lamira
Q-Jay alianza 'muziki wa kidunia' akiwa na kundi la RnB,Wakali Kwanza na kina Joslin,Makamua na wengine kibao na mara ya mwisho walitoa album ya pamoja na Makamua wakiwa chini ya MJ Records na nyimbo zake za kidunia kama Sifai featuring Joslin,na collabo kama Kitu Gani,Nakupa Sifa.

0 comments:

Post a Comment