SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, April 6, 2011

MENGI ATOA UFAFANUZI DHIDI YA KESI YAKE NA YUSUFU MANJI

Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Bw. Reginald Mengi akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Bw. Reginald Mengi ametoa ufafanuzi juu ya kesi ya madai inayomkabili yeye na kituo cha televisheni cha ITV iliyofunguliwa na Bw. Yusufu Manji iliyoripotiwa ndivyo sivyo na baadhi ya magazeti.
Katika taarifa yake Bw. Mengi amesema si sahihi kuandika katika magazeti maneno kama ‘Mengi agonga ukuta’ au ‘akwaa kisiki’ na mengine ya aina hiyo kwa sababu hakuna maamuzi yoyote ya kisheria yaliyotolewa na Mh. Jaji Kaijage kuhusiana na mambi yake kwake kama Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.
Aidha amefafanua juu ya maombi yao katika mahakama kuu na majibu waliyopokea, kwa kusema kuwa wakili wake aliandika barua kwa msajili wa mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam ikionyesha mtiririko wa mwenendo wa kesi hiyo tangu ilipofunguliwa.
Amesema kupitia wakili wake walimsihi msajili awasilishe barua hiyo mbele ya Mh. Jaji Mfawidhi ili aweze kuisoma na baadae aitishe jalada la kesi husika ili aipitie na kujiridhisha na uhalali wa maamuzi mbali mbali yaliyotolewa haswa uamuzi wa 11 Februari 2011, uliozikataa nyaraka zilizowasilishwa siku ya kesi kuanza kwa ajili ya utetezi.
Bw. Mengi amesema majibu waliyopewa msajili alimfahamisha wakili wake kuwa maagizo ya Jaji Mfawidhi ni kwamba endapo wana sababu za kutokuwa na imani na hakimu anayesikiliza kesi basi wafanye ombi kwake wakimtaka ajitoe.
Kimsingi Bw. Mengi ametoa ufafanuzi huo kufuatia habari za maombi yao kupotoshwa na baadhi ya magazeti na kuandikwa kwa namna ambayo baada ya kusomwa katika televisheni na radio ilileta usumbufu mkubwa.
Na.MO BLOG TEAM

0 comments:

Post a Comment