SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, April 15, 2011

KIONGOZI WA UPINZANI UGANDA AJERUHIWA KWA RISAS!!

Rais wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda dakta Kziza Besigye amejeruhiwa baada ya kupigwa risasi mkononi wakati jeshi la nchi hiyo lilipokuwa likijaribu kudhibiti maandamano kutoka wilaya ya Wakiso kuelekea jijini Kampala.
Dakta Besigye aliyeratibu maandamano yanayohimiza watu kutembea kwa miguu kuelekea makazini kwa lengo la kupinga kuongezeka kwa bei ya mafuta na vyakula, amejeruhiwa katika mkono wake wa kulia wakati waandamanaji wakitawanyika baada ya polisi kufyatua bomu la machozi.
Polisi walilazimika kufyatua hewani risasi za mipira na mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya zaidi ya waandamanaji elfu moja pamoja na Besigye mwenyewe walipokuwa wakiandamana kuelekea katikati ya mji mkuu Kampala.
WAKATI HUO HUO
Watu 48 wakiwemo watoto 3 wa shule ya awali wamejeruhiwa wakati polisi walipokuwa wakitawanya umati wa watu kuzuia maandamano yaliyopewa jina la ‘walk-to-work katika maeneo ya Kampala, Wakiso na wilaya nyinginezo.
Chama cha Msalaba Mwekundu nchini Uganda kimesema kimefanikiwa kuwatoa majeruhi hao 48 kutoka maeneo mbali mbali ya jiji hilo wakati maandamano ya kupinga ongezeko la bei ya mafuta na vyakula yakizidi kusambaa.
Mkurugenzi Msaidizi wa Mawasiliano wa Chama cha Msalaba Mwekundu Catherine Ntabadde amesema watoto hao wadogo waliokuwa wakilia wa Safari Kindergarten ya Gayaza walikimbizwa katika hospitali ya Mulago.
Amefafanua kuwa kati ya majeruhi wote watatu wamejeruhiwa kwa risasi, akiwemo Dakta Kiiza Besigye, mwanamke mmoja mwenye ujauzito wa miezi 7 aliyejeruhiwa na risasi tumboni na mtu mwingine asiyefahamika aliyejeruhiwa katika paja.
KATIKA HATUA NYINGINE
Jeshi la Polisi nchini Uganda limesema linachunguza mazingira ambayo rais wa chama cha FDC Dkt. Kiiza Besigye alipigwa risasi ya mkono.
Msemaji wa jeshi hilo Judith Nabakooba ameviambia vyombo vya habari kuwa Dkt. Besigye aliyekuwa katikati ya vurugu wakati polisi wakitawanya maandamano amejeruhiwa kwa risasi ya mpira.
Nabakooba amesema mapema kabla ya kujeruhiwa na risasi hiyo, polisi huko Kisangati kisheria walimtaka kiongozi huyo asiendelee kutembea na maandamano ya watu ambao alisharipoti kuwakusanya.
KWA UPANDE WA SERIKALI
Serikali ya Uganda imesema viongozi wa kisiasa wa upinzani wamekuwa wakipanga kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani ili nchi hiyo ionekane kuwa haitawaliki.
Akizungumza bungeni jana, Makamu wa Tatu wa Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani Kirunda Kivejinje amesema kumekuwa na mipango ya makusudi ya upinzani ya kufanya vurugu hata kabla ya uchaguzi mkuu.
Amesema maandamano ya ‘walk-to-work’ yaliyoandaliwa na Dkt. Besigye hayahusiani kwa namna yeyote na kupanda kwa bei ya mafuta ba bidhaa za vyakula.
Na Chanzo: BOFYA

0 comments:

Post a Comment