Ziara ya Ahmedinejad Lebanon
Katika ziara yake ya kwanza nchini Lebanon, Rais Mahmoud Ahmedinejad wa Iran, aliipongeza Lebanon kwa kusimama imara kuhusiana na suala la Israel . Ahmedinejad alikutana na mwenzake wa Lebanon, rais Michel Suleiman, mjini Beirut, baada ya kupewa makaribisho makubwa na watu wa Lebanon hapo jana. Katika hotuba yake, Rais Ahmedinejad aliipongeza Lebanon kwa sababu ya msimamo wake wa kijasiri inapokuja suala Ia Israel. Rais huyo wa Iran alisema wakati umewadia kwa maeneo yote ya Wapalestina, nchini lebanon na Syria kuwa huru. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton, wakati huo huo ameshtumu jaribio la rais huyo wa Iran kutaka kuitia katika msukosuko Lebanon. Bi Clinton alikumbusha namna mambo yalivyokuwa wakati wa vita vya mwaka 2006 kati ya kundi la Hezbollah na Israel vilivyodumu kwa kipindi cha mwezi mmoja, na kusababisha umwagikaji mkubwa wa damu.
0 comments:
Post a Comment