TUNAADHIMISHA SIKU YA MWALIMU NYERERE LEO
MIAKA 11 TANGU KIFO CHA BABA WA TAIFA, ALIYOYACHUKIA NDIYO TUNAYOYATENDA???
MIAKA 11 TANGU KIFO CHA BABA WA TAIFA, ALIYOYACHUKIA NDIYO TUNAYOYATENDA???
Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Rushwa ni wimbo wa sumu tubadilishiani wimbo huu jamani kama Baba wa Taifa alivyopigia kelele suala la RUSHWA.
Rushwa ni wimbo wa sumu tubadilishiani wimbo huu jamani kama Baba wa Taifa alivyopigia kelele suala la RUSHWA.
Leo, Watanzania wanaadhimisha miaka kumi na moja tangu kifo cha muasisi wa Taifa, hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyetutoka Oktoba 14, 1999 katika Hospitali ya Mtakatifu Joseph, jijini London. Wakati huu tunapoadhimisha miaka 11 tangu Mwalimu alipotutoka, nchi yetu ipo kwenye vuguvugu kubwa la kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge hapo Oktoba 31, siku 17 tu baada ya maadhimisho hayo.
Katika kipindi hiki cha kampeni kuelekea uchaguzi mkuu tumeshuhudia ahadi nyingi tamu kweli kweli kutoka kwa wagombea, huku kila mmoja akiwasilisha kwa namna alivyoweza. Mimi sina haja ya kurudia au kunukuu ahadi hizo.
Lakini mimi kama mwananchi wa kawaida nawakumbusha wagombea na wananchi kwa ujumla kwamba, Baba wa Taifa tunayemuenzi hakuwa muongo aliyejaa hadaa za kujipatia uongozi kama baadhi ya wagombea wetu wanavyojinadi sasa kwa kutumia ahadi ambazo hazihitaji elimu kubwa kuzitambua kuwa zina uongo ndani yake.
Wito wangu kwa wananchi ni kwamba tunapaswa kuwachagua viongozi ambao watayachukia kwa dhati mambo ambayo Baba wa Taifa aliyapinga na kuyakemea vikali enzi za uhai wake. Mfano wa mambo hayo ni Rushwa, ukabila, udini, ubaguzi na matumizi mabaya ya madaraka.
0 comments:
Post a Comment