SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, October 9, 2010

Tangazo la uchaguzi Wa viongozi 2010/11 (TSAH)-Hyderabad India
UMOJA WA WANAFUNZI WA KITANZANIA
HYDERABAD-INDIA
(TSAH)
Tunapenda kuwataarifu wanafunzi wote wa Kitanzania, wanaosoma katika vyuo vikuu na taasisi mbalimbali za kitaaluma hapa Hyderabad India, kuwa kutakuwa na uchaguzi mkuu wa viongozi wa Umoja kwa mujibu wa katiba yetu. Wale wote wenye sifa za kuongoza jumuiya yetu, mnakaribishwa kuchukua fomu kwa wajumbe wa tume waliotajwa hapo chini. Ratiba kamili ya zoezi zima ni kama ifuatavyo. 
(a) Kuchukua fomu na kuzijaza 5/09/2010 mwisho wa kurudisha ni 24/10/2010
 (b)Kukutana na Kamati ya uchaguzi ili kukubaliana kanuni za uchaguzi 24/10/2010
( c) Kampeni na maandalizi tarehe 25/10/2010 hadi 31/10/2010 
(d) Tarehe ya uchaguzi ni 31/10/2010 eneo la Sainikpuri-Ukumbi mtajulishwa baadaye. 
Ndugu Watanzania uchaguzi tarehe 31/10/2010 kwa nafasi ya, 
MwenyekitiKatibu, Katibu Mwenezi na Mweka Hazina.
Fomu zinapatikana kwa wajumbe wafuatao: 

                    1.Tabagi,Mwenyekiti +918897943864 Tolichowki .
2.Majinge, Mjumbe +919966954555.
            3.Simbo,Mjumbe +919948460883 Sainikpuri.
                  4.Lipina,Mjumbe +919885186905 Singapore city.
     5. Kulwa,Mjumbe +919618477357 Alwal.
                      6.J. Makwinya,Katibu +919618477428  Tolichowki.
Wale wenye sifa tunaomba mchukue  form mapema na kurudisha kabla ya tarehe 25/10/2010.
Tabagi, Abel
Mwenyekiti wa kamati maalum ya uchaguzi.

0 comments:

Post a Comment