SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, October 13, 2010


India yatangaza sheria kali zaidi ya marufuku ya kutotoka nje eneo ni Kashmir


Serikali ya India imetangaza marufuku ya kutotoka nje katika eneo la Kashmir lililoko chini ya udhibiti wake kwa lengo la kuwadhibiti wanaharakati wa eneo hilo. Vyombo vya habari vimeripoti kuwa maelfu ya askari wa usalama na polisi wa India jana walitawanywa katika mji wa Srinagar na miji mingine muhimu ya eneo hilo la Waislamu. Vikosi hivyo vimepelekwa huko Kashmir kukabiliana na mikusanyiko ya wananchi inayofanyika kupinga hatua ya serikali ya New Delhi ya kumweka kwenye kizuizi cha nyumbani kiongozi wa kupigania uhuru wa Kashmir Sayyid Ali Gilani. Kiongozi huyo amewekewa kizuizi hicho kwa muda wa mwezi mmoja sasa. Wananchi wa Kashmir wanalalamikia pia uhaba wa bidhaa za vyakula na wa mahitaji mengine ya maisha katika eneo hilo. Eneo la Kashmir limegeuka kuwa uwanja wa machafuko na maandamano ya kuipinga serikali ya India baada ya vikosi vya usalama vya serikali ya New Delhi kumuua kwa kumpiga risasi kijana mmoja wa Kikashmir. Hadi sasa watu wasiopungua 110 wameuawa katika machafuko hayo yaliyoanza mwezi Juni.

0 comments:

Post a Comment