Ulimwengu
umeendelea kusikitishwa na kulaani mashambulizi ya manowari za kivita za
utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya msafara wa kimataifa wa meli
zilizobeba misaada ya kibinaadamu kwa ajili Wapalestina wa Ukanda wa
Gaza. Watu zaidi ya 20 wameuawa shahidi na wengine zaidi ya 50
wamejeruhiwa katika hujuma hiyo ya kinyama ya jeshi la utawala haramu wa
Israel unaoungwa mkono kikamilifu na Marekani. Viongozi wa ngazi za juu
wa Iran wameungana na wapenda haki ulimwenguni kote kulani mashambulizi
hayo, ambapo nchini Uturuki mamia ya wananchi wa nchi hiyo wameandamana
kwenye miji ya Istanbul, Ankara na mkabala na ubalozi wa Israel kulaani
tukio hilo huku wakipiga nara za kupinga Israel. Nchi za Lebanon, Iraq,
Jordan, Belgium, Pakistan, Ujerumani, Misri, Ufaransa, Qatar na
nyinginezo duniani zimelaani vikali mashambulizi hayo. Amru Mussa Katibu
Mkuu wa Umoja wa nchi za Kiarabu amelaani mashambulizi hayo
yaliyofanyika leo na kusema kuwa, kushambulia msafara wa misaada ya
kibinaadamu ni jinai kubwa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa nchini
Uganda amesema kwamba, ameshangazwa na mashambulizi hayo na kuhukumu
hatua hiyo ya kinyama.
|
0 comments:
Post a Comment