Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International
linasema ulimwengu haufanyi juhudi za kutosha kuendeleza haki,
huku mamilioni ya watu wakikabiliwa na hujuma, mateso na umaskini.
Katika ripoti yake ya mwaka kuhusu haki za binadamu duniani,
shirika hilo limezilaumu serikali mbalimbali kwa kuzuia maendeleo
katika kulinda haki za binadamu kwa kukataa kujiunga na mahakama
ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC mjini The Hague Uholanzi, au
kwa kuwalinda washirika wao wasifikishwe mbele ya vyombo vya
sheria. Shirika la Amnesty International limezikosoa Urusi na China
kwa ukiukaji wa haki za binadamu. Limemkosoa pia rais wa Marekani
Barack Obama kwa kushindwa kuifunga jela ya Guantanamo. Shirika
hilo limesema mwaka wa 2009 ulikuwa muhimu kwa haki ya kimataifa
kwa sababu mahakama ya ICC ilitoa waranti wa kukamatwa rais wa
Sudan Omar Hassan al Bashir kwa uhalifu dhidi ya binadamu na
uhalifu wa kivita.
Deutsche Welle.
Deutsche Welle.
0 comments:
Post a Comment