
JK akiwa katika picha ya pamoja na Wah. Majaji wa
Afrika Mashariki baada ya kufungua mkutano wao jana hoteli ya Ngurdoto
jijini A-Taun
Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Augustine Ramadhani akiwa na
mdau Emmanuel Mamuya aliyekuwa refa wa mpambano wa soka kati ya Wah.
Majaji wa Kenya na Tanzania kwenye uwanja wa Ngurdoto baada ya mkutano.
Mdau Mamuya ni meneja wa IT na mikutano hapo hotelini. Mh Jaji mkuu ni
mpenzi sana wa michezo. Yeye ni mlezi wa chama cha Basketball nchini na
enzi zake aliwahi kucheza sana mchezo huu hadi timu ya taifa
Mh. Jaji Bernard Luanda wa Tanzania akipiga free kick
wakati wa gemu dhidi ya Kenya. Ikumbukwe Mh. Luanda keshapigia Taifa
Staras na Simba akiwa kiungo hodari sana. Hadi leo yuko fiti ila basi tu
majukumu yamemtinga. Katika mchezo huu Tanzania ilishinda 3-0
Gemu linaendelea, ila timu zote zilikuwa zimevaa jezi
rangi moja na mshabiki aliye pembeni anajaribu kujaji nani ni wa timu
gani hapo. wenyewe walielewana bila shida
Harambee Judges Stars
Taifa Judges starsMichuzi.com




0 comments:
Post a Comment