Mwanamuziki wa Uingereza Elton
John anatarajiwa kuwepo katika tamasha nchini Morocco licha ya kuwepo
wito wa kuzuiwa.
Wapiganaji wa kiislamu wamejaribu kuzuia mwaliko
wake huo, wakidai kuwa mwanamuziki huyo aliyeweka wazi kuwa anafanya
mapenzi ya jinsia moja anaenda kinyume na maadili ya umma.Lakini waratibu wa tamasha la Mawazine huko Rabat wametetea uamuzi wa kumwalika John, kwa madai ya "kustahamiliana kimaadili".
Mkurugenzi wa sanaa wa tamasaha la Mawazine Azizi Daki ameiambia BBC kuwa wanatarajia umati mkubwa kujitokeza kwenye oneysho lake.
Amesema, " Kawaida umati mkubwa ni takriban watu 40,000."
" Usiku wa leo tunatarajia takriban watu 60,000 kuja kumwona Elton John."
Bw Daki amesema hii ni mara ya kwanza kwa John kufanya onyesho Morocco na ana umaarufu sana nchini humo.
Amesema, " Kipaji chake kimekuwa cha kuridhisha sana, anawafanya raia wa Morocco wawe na matumaini na kila mmoja anajua nyimbo zake."
Wasanii maarufu
Lakini mapema mwezi huu, chama cha Islamist
Justice and Development (PJD) lilipinga onyesho hilo la John.
Mwanachama wa PJD Mustapha Ramid amesema: " Tuliiomba serikali kutomhusisha mtu huyo katika orodha ya wasanii walioalikwa kwenye tamasaha hilo."
"Mwanamme huyu-samahani, bora niseme mtu huyu, na si mwanamme huyu- anajulikana kwa kujisifu kwa kufuata mapenzi ya jinsia moja."
Bw Ramid amesema, "Morocco ni taifa la kiislamu ambapo jukwaa halitakiwi kumruhusu mtu mwenye kiwango hicho cha ufisadi kufanya onyesho kwasababu inabidi tuwanusuru watoto na mambo kama hayo."
Tamasha la Mawazine la siku tisa huhusisha wasanii kutoka duniani kote, wakiwemo Sting, Carlos Santana, Julio Iglesias, Toumani Diabate na Alpha Blondy.
Makundi ya kiislamu yamekuwa yakikosoa tamasha hizo kwa kushinikiza ufisadi na kuharibu maadili ya kiislamu.
Mwezi Februari, John aliliambia jarida la America's Parade: " Nafikiri Yesu alikuwa mtu mwenye imani, mtu hodari sana mwenye kufuata mapenzi ya jinsia moja aliyeelewa matatizo ya mwanadamu."
Kauli hii ndio ilisababisha tamasha lake lililokuwa lifanyike Mei 18 kuzuiwa.
BBC Swahili.

0 comments:
Post a Comment