SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, May 12, 2010

David Cameron Waziri Mkuu mpya Uingereza

David Cameron akikutana na Malikia Elizabeth wa Uingereza.
David Cameron amepokea rasmi wadhfa wa Waziri Mkuu baada ya kukutana na Malikia Elizabeth wa Uingereza.
Kiongozi wa chama cha Conservative, David Cameron, ndiye Waziri Mkuu wa Uingereza baada ya Gordon Brown kujiuzulu Jumanne jioni.
Bw Cameron, mwenye umri wa miaka 43, aliingia makazi rasmi ya Waziri Mkuu wa Uingereza, 10 Downing Street, baada ya kuzuru Buckingham Palace, makazi ya Malikia wa Uingereza kwenda kupokea rasmi pendekezo la kumtaka aunde serikali mpya.
Alisema anakusudia kuunda "mseto kamili" na chama cha Liberal Democrats kuunda serikali imara na yenye utulivu".
Chama chake ndicho kilipata idadi kubwa zaidi ya viti bungeni katika uchaguzi uliofanyika juma lililopita, ingawa hakikupata uwingi unaotakiwa kuunda serikali bila kushirikiana na vyama vingine.

0 comments:

Post a Comment