SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, May 4, 2010

Dunia sasa inaelekea wapi jamani?

Aua mtoto wa kufikia kwa kupika mbegu
Polisi wilayani Mpanda inamshikilia mkazi wa Kijiji cha Lwega, Nuwa Shema (30) kwa tuhuma za kumuua mwanawe wa kufikia na kisha kumzika kwa siri.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Isunto Mantage alisema tukio hilo lilitokea Februari 8 mwaka huu .

Mzazi huyo alimuua mtoto huyo, Tedy Paschal (6) baada ya kupika kunde zinazodaiwa kuhifadhiwa na mtuhumiwa huyo kwa ajili ya mbegu.

Mantage aliliambia gazeti hili kwamba mtuhumiwa alianza kumshambulia kwa fimbo na kisha kumfunga kamba na kumning’iza juu ya mti uliopo nje ya nyumba yao.

Kwa mujibu wa Kamanda, mvua kubwa ilimnyeshea mtoto akiwa amenin’gizwa mtini jambo lililosababishia kupoteza uhai wake. Inadaiwa baba huyo wa kufikia aliuchukua mwili na kuuzika mbele ya nyumba yake.

Inadaiwa alimtishia mama wa mtoto huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja kuwa endapo angetoa siri hiyo naye angeuawa jambo lililovumiliwa na mama huyo kwa kipindi chote hicho.

Kamanda Mantage alisema kuwa Aprili 28 mwaka huu majirani walianza kudadisi kutoonekana kwa mtoto huyo ambapo mama huyo aliangua kilio jambo lililosababisha majirani kupata hofu na kumbana zaidi.

Ndipo mama huyo alipowaeleza majirani zake chanzo cha mtoto wake kutoonekana na majirani hao kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi na kisha mtuhumiwa huyo kukamatwa.

0 comments:

Post a Comment