SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, May 4, 2010

Albino wawili wauawa Burundi


Watoto albino
Mauaji ya Albino bado yanaendelea Burundi.
Watu waliokuwa wamejihami kwa mapanga wamemuua mwanamke Albino na mtoto wake wa miaka minne nchini Burundi.

Inaarifiwa kuwa maiti za wawili hao ilikatwakatwa vibaya katika mkoa wa Cankuzo, unaopakana na Tanzania.
Mwenyekiti wa chama cha maalbino nchini humo, Kassim Kazungu, ameelezea BBC kuwa anashuku wauaji walitoroka gerezani na walikuwa wamehukumiwa kwa makosa ya kuwashambulia maalbino.

Aliongeza kuwa shambulio kama hilo halijashuhudiwa Burundi katika kipindi cha mwaka mmoja.

Baadhi ya watu wanaamini kuwa viungo vya mwili wa albino vinaweza kuwatajirisha.

0 comments:

Post a Comment