Pages

Tuesday, March 22, 2011

TAARAB YAPATA PIGO KUBWA!!

Mwimbaji wa taarab Issa kijoti enzi za uhai wake.
Kikundi cha taarabu cha Five Stars kimepata pigo baada ya kufiwa na jumla ya wanakikundi 10,
wakiwemo waimbaji, mafundi mitambo na mkurugenzi wa bendi. Katika ajali ya gari iliyotokea usiku
wa kuamkia leo Mikumi, Mkoani Morogoro, wakitokea Kyela,Mbeya ambako walikuwa na ziara ya
kimuziki. Katika ajali hiyo, alikuwemo pia mwimbaji mkongwe Mwanahawa Ally ambaye alinusurika
baada ya kuumia vibaya, aliungana nao kama mwimbaji mwalikwa akitokea Melody ModernTaarab. Pia
mwanamuziki mwingine mahiri, Hammer Q, ambaye alikuwepo kwenye msafara, alinusurika baada ya
kubaki Iringa wakati wenzake wakiendelea na safari. .
Yafutayo ni majina ya wana Five Stars waliothibitishwa kufa hadi sasa:
Issa kijoti - mwimbaji
Husna mapande-mwimbaji
nasoro madenge - mkurugenzi
Sheba juma - mpiga solo
Omari hashimu- mpiga bass
Omari tall- fundi mitambo
Hamisa mussa - mwimbaji
Rama kinyoya - mwimbaji
Tizo mgunda - mcheza shoo
Haji mzaniwa - fundi mitambo

No comments:

Post a Comment