Pages

Wednesday, May 26, 2010

Watu 30 wauwawa Jamaika

KINGSTON
Watu wasiopungua 30 wameuwawa kwenye mapambano kati ya wafuasi wa mlanguzi wa dawa za kulevya na vikosi vya usalama katika mji mkuu wa Jamaica, Kingston. Maafisa wanajaribu kumkamata Christopher Coke ambaye anatakikana na Marekani kujibu mashtaka ya ulanguzi wa madawa ya kulevya na silaha.
Inaaminiwa kwamba Coke anajificha katika kitongoji cha Tivoli Gardens mjini Kingston ambako wafuasi wake wameweka vizuizi kuwazuia maafisa wa usalama wanaotaka kumtia mbaroni. Serikali imetangaza hali ya hatari katika baadhi ya maeneo ya mji mkuu Kingston kutokana na machafuko yaliyozuka.
Deutsche Welle.

No comments:

Post a Comment