SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, October 9, 2013

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Suedi Kagasheki ametangaza kuanza rasmi kwa msako wa wafanyabiashara wa sekta ya utalii (Makanjanja) wanaofanya biashara kinyume na taratibu.

Mwenyekiti na Wajumbe wateule Mamlaka ya wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Suedi Kagasheki (MB) (wapili kutoka kulia kwa waliosimama msitari wa mbele) mara baada ya kuzinduliwa rasmi katika Ukumbi wa Ngorongoro ulioko Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dar es salaam
Wenyeviti na Wajumbe wateule wa vyombo vitatu, Bodi ya Leseni za Biashara za Utalii Tanzania, Mamlaka ya Rufaa na  Kamati ya Ushauri wa Kitaalam wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Suedi Kagasheki (MB) (wanne kutoka kulia kwa waliosimama msitari wa mbele) mara baada ya kuzinduliwa rasmi katika Ukumbi wa Ngorongoro ulioko Maqkao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dar es salaam.
--
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Suedi Kagasheki (MB) ametangaza kuanza rasmi kwa msako wa wafanyabiashara wa sekta ya utalii (makanjanja) wanaofanya biashara kinyume na taratibu.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Leseni za Biashara za Utalii Tanzania, Mamlaka ya Rufaa na Kamati ya Ushauri wa Kitaalam vya Wizara alisema, serikali imeamua kupambana na wafanyabiashara wa sekta ya utalii wanaoikosesha mapato kwa kufanya biashara hiyo kinyume na taratibu.

 “Leo ninazindua Bodi ya Leseni za Biashara za Utalii Tanzania inayoundwa na watu makini, watu ambao hawawezi kusukumwa na rushwa ndogo ndogo ili kuziba mianya yote ambayo inasababisha serikali kukosa mapato. Hivyo kupitia bodi hii, sasa mfanyabiashara na serikali wote watapata faida,” alisema Mhe. Kagasheki.

Aidha aliongeza kuwa, hivi sasa leseni nyingi zimekwisha muda wake na hivyo wafanyabishara wanalazimika kuomba upya na hapo ndipo vyombo hivyo vipya vitakapoanza msako kwa kutekeleza majukumu yake ya kusaidia katika usimamizi, kutoa miongozo na ushauri wa kitaalam kulingana na sera na sheria.

Mhe. Kagasheki aliongeza kuwa, kuundwa kwa vyombo hivyo ni suluhisho katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya utalii nchini.
Na Haki Ngowi

0 comments:

Post a Comment