SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, October 10, 2013

SPF YAWAOMBA WASANII, WANAMICHEZO KUJIUNGA NA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI‏

Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Costantina Martin.
Elizabeth Michael (Lulu) na Flaviana Matata.

Steve Nyerere.
====
Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Costantina Martin anasema lengo kukukutana na wadau hawa ni kutambulisha kwao mpango wa uchangiaji wa hiari (PSPF SUPPLIMENTARY SCHEME-PSS) ambao unamwezesha mtu yeyote kujiunga na mpango huo awe ameajiriwa au amejiajiri mwenyewe. “Uzuri wa mpango huu wa uchangiaji wa hiari, unaruhusu hata wanachama waliokwenye mifuko mingine kujiunga nao lakini pia mwanachama anayohiari ya kuhamia kwenye mpango wa uchangiaji kwa mujibu wa sheria yaani
Main Scheme” Anasema Costantina
Anasema kuwa kiasi cha michango kwenye mpango wa hiari kinaanzia shilingi elfu kumi (10,000) kwa mwezi na hakuna kiwango cha juu ambapo mwanachama yuko huru kuchagua kuwasilisha michango kwa wiki, mwezi au
kwa msimu na michango hiyo inawasilishwa kupitia akaunti ya benki, au wakala wa malipo wa M-Pesa na Airtel Money.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu anasema mpango wa hiari ni mkombozi kwa wadau wa sanaa na michezo kwa kuwa utawawezesha kujiwekea akiba itakayowasaidia wakati na hata baada ya kustaafu kufanya shughuli zao.
Katika kuhakikisha kuwa elimu ya uhifadhi inawafikia watu wengi na kuwahamasisha kujiunga na mpango huo waa hiari PSPF imekusudia kuwafanya wasanii na wanamichezo kuwa mabalozi katika kufikisha elimu hiyo kwa
jamii. “Sio jambo rahisi kuielimisha jamii juu ya kujiwekea akiba kwa ajili ya maisha yao ya baadaye lakini kupitia wasanii na wanamichezo tunaweza kuleta mabadiliko na kufanya watu wengi kuwekeza katika mifuko ya
hifadhi ya jamii” anasema Mayingu Shuhudia picha za tukio zima la hafla ya chakula cha mchana kwa wadau wa sanaa na michezo iliyoandaliwa na PSPF.
Wadau wa sanaa.
 Afisa Mahusioano wa PSPF, Fatma Elhagy akiwa na mtumishi mwenzake.
 Afisa Mawasiliano na Masoko wa PSPF, Hawa Kikeke.
Nilipopokea mwaliko kutoka Mfuko wa Pensheni (PSPF) ukiniomba kuhudhuria kwenye hafla fupi ya chakula cha mchana pamoja na wadau wa tasnia ya sanaa na michezo nchini, sikuelewa mara moja lengo la hafla hiyo lakini baada ya kufika ukumbini na kupata ufafanuzi wa mabadiliko makubwa yaliyofanywa na PSPF nikapata somo.
Kumbe PSPF sasa si kwa watumishi wa umma pekee bali hata wanamuziki, waigizaji, wachezaji na hata watu wengine waliokwenye sekta zisizo rasmi wanaweza kujiunga na kufaidika na mafao yanayotolewa na mfuko huo.
Wadau wengi wa tasnia ya sanaa na michezo walijitokeza kwenye halfa hiyo tukianza na Elizabeth Michael Lulu, Mwanamitindo mwenye mafanikio makubwa ndani na nje ya nchi, Flaviana Matata, Mtitu, Steve Nyerere, Nahodha wa timu ya taifa ya soka wanawake Sophia Mwasikili na wadau wengine wengii.
 Naibu Mkurugenzi wa Michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Juliana Yasoda.
Mdau wa sanaa na akiwa na staa wa kesho.
Wadau wa sanaa na michezo.
 Baadhi ya watumishi wa PSPF.
 Mshereheshaji katika hafla hiyo, Angela Bondo.
 Baadhi ya mameneja na wakurugenzi wa idara mbalimbali wa PSPF.
Wadau.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa miguu kwa wanawake, Amina Karuma akiwa na Nahodha wa timu ya Taifa ya soka kwa wanawake Sophia Mwasikili.
 Elizabeth Michael (Lulu) na Flaviana Matata.
 Mr. Tairo kutoka Bodi ya Filamu Tanzania.
 Mdau.
Kocha msaidizi wa klabu ya Simba Jamuhuri Kiwelu Julio nae alikuwepo.
 Columba Samjela kutoka Umoja wa Washereheshaji.
 Meneja Matekelezo wa PSPF, Amin Labani.
Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji PSPF, Frances Mselemu.
 Muda wa maakuli.
 Mwendo ni 'kujisevia'.
 Wadau wa sanaa na michezo.
 Baadhi ya watumishi wa PSPF katika picha ya pamoja.
 
CHANZO NA GPL

0 comments:

Post a Comment