SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, October 9, 2013

MUME AMUUA MKEWE KWA KIPIGO




Kitambulisho cha kura cha Marehemu Bi Rahima Ali Gendo ambaye alipigwa na mumewe hadi kupelekea kifo chake.
Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live Joyce Kiria akizuru kaburi la marehemu Rahima.
rahima3  Balozi wa nyumba kumi wa eneo hilo ambako Bi Rahima alifariki akifanya mahojiano na Mtangazaji wa kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa na EATV. Kesi za unyanyasaji dhidi ya wanawake zinazidi kuwa nyingi. 

Kesi za unyanyasaji dhidi ya wanawake zinazidi kuwa nyingi
Wanawake wameendela kuumizwa na ubabe wa waume zao. Hivi karibuni, katika kijiji cha Kizanda wilayani Lushoto mkoa wa Tanga, mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Bi. Rahima alifariki dunia baada ya kupigwa na mumewe mateke ya tumboni angali mja mzito. 

Taarifa za awali kutolewa zinasema kuwa mwanamke huyo alifariki kutokana na homa, lakini ndugu wa marehemu wamedai kuwa kifo cha ndugu yao kimetokana na kipigo. 
Bi Rahima ambaye alikuwa ni mja mzito, alifariki mwezi wa saba mwaka huu. 

Taarifa za awali ambazo zilifikia Wanawake Live na Super Woman Joyce Kiria kufuatilia zilionekana kupita EATV usiku wa juzi, na pia unaweza kufuatilia kwenye YouTube kupitia linki hii hapa chini ili ufahamu kile wanasheria wamekizungumza katika kutafuta haki kufuatia suala hili ambalo hata viongozi w a kijiji hicho wameshindwa kulitatua.

0 comments:

Post a Comment