Mratibu wa taifa wa utepe mweupe wa
Uzazi salama Tanzania Mama Rose Mlay akizungumza katika Mkutano wa siku
moja kati ya Uongozi wa Mkoa wa Rukwa, viongozi wa dini, wabunge,
viongozi wa asasi za kijamii na za kidini na Muungano wa utepe mweupe wa
Uzazi wa Salama Tanzania katika ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga tarehe
8 Oktoba 2013. Akielezea malengo ya mkutano huo alisema Serikali ya
Tanzania inaheshimu ahadi yake ya kuwa na asilimia hamsini ya vituo vya
afya Mkoani Rukwa vitakavyotoa huduma kamili za dharura za uzazi zikiwa
ni pamoja na upasuaji kumtoa mtoto na kutoa damu salama zinapohitajika
ifikapo 2015. Ktikati ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Ndugu
Samson Mashalla.
Vikundi kazi katika kujadili mpango mkakati utakaotumiwa kuendeleza umuhimu wa huduma za uzazi salama katika jamii.
Dkt. Lunyelele akichangia moja ya mada katika Mkutano huo.
Picha ya pamoja
Chakula cha pamoja.Picha na Hamza Temba
- Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
0 comments:
Post a Comment